Naibu Spika wa Bunge, Daniel Baran Sillo, amesema Bunge lipo tayari kushirikiana na Serikali katika maandalizi ya AFCON PAMOJA 2027. Alitoa kauli hiyo wakati wa Bonanza la Bunge na NMB jijini Dodoma, lililoandaliwa na NMB Bank kwa kushirikiana na Bunge.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alisema benki hiyo imeandaa bonanza hilo kwa sababu michezo ina mchango katika afya na tija ya viongozi na watumishi. “Tunataka michezo iwe sehemu ya utamaduni wa kazi na huduma kwa wananchi,” alisema.
Mwenyekiti wa Bonanza la Bunge na Mbunge wa Makete, Festo Sanga, alisema tukio hilo limewakutanisha wabunge, wizara na taasisi mbalimbali, huku likitumika kuhamasisha mazoezi na mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Machano Ali Machano, alisema mashindano ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayofanyika Arusha Desemba 2026 yatakuwa hatua nyingine ya kuimarisha michezo na ushirikiano wa kikanda.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...