Benki ya NMB imekabidhi hundi ya udhamini kwa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya Maonesho ya Nanenane 2026, ikiendeleza ushirikiano wake wa muda mrefu na Serikali katika kukuza sekta ya kilimo.
Makabidhiano yaliyofanyika jana jioni jijini Dodoma yamefikisha jumla ya udhamini wa NMB katika maonesho hayo hadi Sh572 milioni ndani ya miaka minane mfululizo, yakionyesha dhamira ya benki hiyo katika kusaidia maendeleo ya wakulima, wafugaji na wavuvi.
Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango, alisema Nanenane ni jukwaa muhimu la kuwafikisha wazalishaji kwenye maarifa, teknolojia na huduma za kifedha zinazoongeza tija na kufungua fursa mpya za biashara.
Waziri wa Kilimo Daniel Chongolo aliipongeza NMB kwa kuendelea kuwa karibu na wakulima na kuitaka benki hiyo kuendeleza ushirikiano huo ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi kupitia elimu, teknolojia na huduma za kifedha.
Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo (wapili kushoto), akipokea mfano wa hundi ya udhamini kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango (wapili kulia), wakati wa hafla iliyofanyika jana jioni jijini Dodoma kwa ajili ya Maonesho ya Nanenane 2026. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli, na kulia ni Meneja Mwandamizi wa Idara ya Biashara za Serikali wa NMB, Amanda Feruzi. Udhamini huo unaendeleza ushirikiano wa muda mrefu kati ya NMB na Serikali katika kukuza maendeleo ya sekta ya kilimo.




.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...