Na Janeth Raphael - MichuziTv
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewapa muda wa wiki moja wamiliki na waendeshaji wa kampuni za mabasi makubwa ya mikoani kuhakikisha wanaanza kutumia Stendi ya Magufuli kama kituo cha kuanzia na kumalizia safari zao, katika hatua inayolenga kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Chalamila ametoa agizo hilo leo jijini Dar es katika Mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema mabasi hayo hayatapaswa tena kuingia katikati ya jiji kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria, isipokuwa kampuni sita ambazo tayari zimepewa vibali maalum vya kushusha abiria katika maeneo ya katikati ya jiji.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa, kampuni nyingine zote zinatakiwa kutumia Stendi ya Magufuli na kuzingatia utaratibu mpya uliowekwa na Serikali.
Chalamila amesema wamiliki na waendeshaji wa mabasi hayo wametakiwa kutumia muda uliopo hadi Agosti 17, 2026 kufanya maandalizi muhimu, huku utekelezaji wa agizo hilo ukianza rasmi baada ya tarehe hiyo.

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuboresha mfumo wa usafiri na kupunguza msongamano unaoendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Ameeleza kuwa mabasi makubwa yanapoingia katikati ya jiji kwa ajili ya kushusha au kupakia abiria, yanaongeza idadi ya magari katika maeneo ambayo tayari yana msongamano mkubwa, hivyo matumizi ya Stendi ya Magufuli yatasaidia kuyapunguza mabasi hayo katika maeneo ya katikati ya jiji na kuweka utaratibu mzuri wa usafirishaji wa abiria wanaoingia au kutoka Dar es Salaam.
Chalamila amesema abiria watakaofikishwa katika Stendi ya Magufuli hawataachwa bila usafiri wa kuendelea na safari zao, kwani wataweza kutumia huduma mbalimbali za usafiri wa ndani kuelekea maeneo wanayokwenda.

Miongoni mwa usafiri huo ni mabasi ya mwendokasi, daladala, bajaji na pikipiki, huku kampuni za mabasi zikiruhusiwa pia kuweka huduma za shuttle kwa ajili ya kuwasaidia abiria kutoka stendi hiyo kwenda maeneo mbalimbali ya jiji.
Kwa mujibu wa Chalamila, utaratibu huo hautalenga tu kupunguza msongamano wa magari, bali pia unalenga kulinda na kuongeza fursa za ajira na biashara kwa waendeshaji wa usafiri wa ndani.

Amesema mabasi makubwa yanapoingia hadi katikati ya jiji na kufanya shughuli ambazo zinaweza kufanywa na watoa huduma za usafiri wa ndani, yanaathiri moja kwa moja shughuli za kiuchumi za kundi hilo la wadau.
Amesema mfumo huo mpya utawezesha kuwepo kwa mgawanyo mzuri wa majukumu katika sekta ya usafirishaji, ambapo mabasi makubwa yatabeba abiria kutoka mikoa mbalimbali na kuwafikisha katika Stendi ya Magufuli, kisha usafiri wa ndani kuchukua jukumu la kuwaunganisha abiria hao na maeneo mbalimbali ndani ya Dar es Salaam.
Chalamila amewataka wamiliki na waendeshaji wa mabasi makubwa kutumia muda uliotolewa kufanya maandalizi ya kutosha, ikiwemo kupanga namna ya kuwasaidia abiria wao kuendelea na safari kutoka Stendi ya Magufuli.

Amesisitiza kuwa baada ya Agosti 17, 2026, utekelezaji wa utaratibu huo utaanza rasmi, huku kampuni ambazo hazina vibali maalum vya kushusha abiria katikati ya jiji zikitarajiwa kuzingatia kikamilifu agizo hilo.
Hatua hiyo inatarajiwa kuwa sehemu ya mabadiliko katika mfumo wa usafiri wa Mabasi ya masafa marefu jijini Dar es Salaam, huku Serikali ikilenga kuhakikisha mabasi makubwa yanafanya shughuli zake katika vituo vilivyotengwa na abiria wanapata huduma rahisi na salama za usafiri wa ndani kuelekea wanakokwenda.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...