Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais–Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Mb), Ridhiwani Kikwete, amezitaka shule za msingi na sekondari kuwa na karakana zitakazokuwa chemchemi za ubunifu kwa vijana, huku akisisitiza kazi zitakazobuniwa zisajiliwe ili wabunifu wanufaike nazo.

Ridhiwani amesema usajili huo utawasaidia vijana kumiliki kazi zao na kuzitumia kama fursa za kiuchumi, badala ya watu wengine kuchukua mawazo yao na kujinufaisha huku wabunifu wakibaki bila manufaa.

Amesema hayo akimwakilisha Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, katika kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Taasisi ya Baobab, iliyopo Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani.

Mkurugenzi wa Baobab, Shani Swai, amesema kwa sasa shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 1,000 na tangu mwaka 2007 hadi 2026, jumla ya wanafunzi wa 4,495 wa kidato cha sita wamehitimu, huku asilimia 98 wakiendelea na elimu ya vyuo vikuu ndani na nje ya nchi na wanafunzi 3,270 wamehitimu kidato cha nne ambapo asilimia 95 wameendelea na sekondari na vyuo vya ufundi. 

Naye Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Lyabwene Mtahabwa, amewataka Watanzania kushikamana katika kuwalinda .

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...