Na Mwandishi wetu, Simanjiro
MDAU wa maendeleo wa Mkoa wa Manyara, Taiko Ole Kulunju ameongoza harambee ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Noomunyi kijiji cha Loiborsiret Wilayani Simanjiro na kupatikana shilingi milioni 71,050,000.
Taiko akizungumza kwenye harambee hiyo amewapongeza wakazi wa vitongoji vyote vya kijiji cha Loiborsiret kwa kujitoa kwa moyo mmoja katika kuchangia ujenzi wa madarasa ya shule mpya ya Noomunyi.
"Nawashukuru Diwani wa Kata yetu Mhe Ezekiel Lesenga Mardadi, mjomba wangu Edward Loure wa UCRT, Lamnyaki Lazaro na mgeni wetu Paulo kutoka Wilaya ya Monduli na watu wote wa Loiborsiret, kwa kutuunga mkono kwenye harambee hii," amesema Taiko.
Amesema kukamilika kwa madarasa ya shule hiyo itakuwa vyema kwa wanafunzi wa eneo hilo kusoma karibu kwani wanaotembea umbali mrefu kufuata elimu ya msingi.

Diwani wa kata ya Loiborsiret Ezekiel Lesenga (Mardadi) amewapongeza wadau mbalimbali na wananchi wa eneo hilo kwa mchango wao.
Mardadi ameeleza kwamba ataishirikisha Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro ili nao wachangie ujenzi wa madarasa mengine ya shule hiyo mpya iliyojengwa kwa nguvu za jamii.
Mratibu wa shirika lisilo la kiserika la Ujamaa Community Resource Team (UCRT) Edward Loure amesema amefanikisha ujenzi wa madarasa mawili ya shule hiyo.
Loure ameiasa jamii ya eneo hilo kuweke juhudi kubwa katika kuzingatia elimu ya watoto wao na kutunza ardhi ambayo ni urithi wa eneo hilo.
"Kila wakati nimekuwa nikisema kuwa our land is our life (ardhi yetu ndiyo maisha yetu hivyo tuilinde ardhi yetu kwa manufaa ya watoto wetu na mifugo yetu," amesema Loure.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...