Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (katikati), pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu ya soka ya benki hiyo, wakishangilia mara baada kupokea kikombe kutoka kwa Mweka Hazina wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) , Bw. Rayson Foya, baada ya kuibuka na ushindi kwa kuichapa timu ya benki ya Mwanga Hakika kwa bao 1-0 katika mchezo wa fainali za Ligi ya Chama TBA, katika Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser ( wa tatu kushoto), akipokea kikombe kutoka kwa Mweka Hazina wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) , Bw. Rayson Foya( wa pili kushoto) baada ya timu ya benki hiyo, kuibuka mshindi kwa kuichapa timu ya benki ya Mwanga Hakika kwa bao 1-0 katika mchezo wa fainali za Ligi ya Chama cha Mabenki Tanzania (TBA Footie Tournament 2026), katika Viwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania , Bw. Paschal John ( kushoto) akipokea tuzo ya mchezaji bora kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA), Bw. Dan Tandasi mara baada ya mchezo wa fainali za Ligi ya Chama cha Mabenki Tanzania (TBA Footie Tournament 2026), uliyofanyika katika Viwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam jana.
Picha mbalimbali zikionesha mtifuano mkali dhidi ya wachezaji wa timu za soka za benki ya Absa na Mwanga Hakika, katika mchezo wao wa fainali za Michuano ya TBA Footie Tournament 2026, katika Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam jana. Absa ilishinda mtanange huo kwa bao 1-0 hivyo kutwaa ushindi wa michuano hiyo kwa mwaka huu.
Kikosi kabambe cha timu ya soka ya Benki ya Absa, wakipiga picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo wa fainali dhidi ya Mwanga Hakika Bank, katika Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam jana. Absa ilishinda kwa bao 1-0.










Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...