Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MBUNIFU wa Mashine ya Kuchanganya Chakula cha Mifugo kutoka Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Songea, Mwalimu Sussack Mbulu, amesema mashine hiyo ni mkombozi kwa wafugaji katika kuandaa chakula bora cha mifugo na kuongeza thamani ya mifugo yao sokoni.
Mwalimu Mbulu ameyasema hayo katika Viwanja vya Dkt. John Samwel Malecela jijini Dodoma, ambako yanaendelea Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Kitaifa.
Amesema mashine hiyo ni miongoni mwa ubunifu unaolenga kurahisisha shughuli za ufugaji, ambapo inaweza kuchanganya chakula cha mifugo kwa uwezo wa kilogramu 480 kwa saa.
“Mashine hii itamsaidia mfugaji kurahisisha maandalizi ya chakula cha mifugo na kuhakikisha anapata chakula kilichochanganywa vizuri, hivyo kuongeza ufanisi katika ufugaji,” amesema.
Mwalimu Mbulu amesema mashine hiyo inauzwa kwa Shilingi 400,000, huku wananchi wakihitaji ya wanaweza kufikiwa popote walipo.
Amewataka wafugaji kutumia teknolojia na ubunifu huo ili kurahisisha kazi, kuongeza uzalishaji na kuwawezesha kufuga mifugo kwa wingi yenye tija na inayoweza kuingia katika masoko.
Mbali na mashine hiyo, amesema VETA Songea imebuni pia kifaa cha kumwagilia mashamba (Sprinkler) ambacho kina uwezo wa kumwagilia eneo la robo ekari ndani ya dakika 15.
Aidha, amewataka wananchi na wafugaji kutembelea Banda la VETA katika maonesho hayo ili kupata elimu kuhusu teknolojia za kilimo na ufugaji, pamoja na kupata taarifa kuhusu fursa za kujiunga na masomo katika vyuo vya VETA vilivyopo nchi nzima.




.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...