Na Mwandishi Wetu, Tanga
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), CPA Anthony Kasore, amesema mamlaka hiyo imeweka mkakati wa kutoa mafunzo ya ufundi na ujuzi kwa vijana ili kuwafungulia fursa za ajira na kujiajiri katika sekta mbalimbali.

CPA Kasore ameyasema hayo alipotembelea Banda la VETA katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara jijini Tanga.

Amesema VETA ina vyuo katika mikoa mbalimbali nchini, hivyo vijana wanapaswa kutumia fursa hiyo kujiunga na vyuo hivyo na kupata ujuzi unaowawezesha kukabiliana na mahitaji ya soko la ajira.

“VETA imejenga vyuo katika kila mkoa na wilaya zake kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi wa maeneo husika, ili kuhakikisha changamoto zao zinapatiwa ufumbuzi kupitia elimu na mafunzo ya ufundi stadi,” amesema CPA Kasore.

Aidha, amesema gharama za mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma kozi ndefu ni Sh 60,000 kwa mwaka kwa wanafunzi wa kutwa, huku wanafunzi wa bweni wakilipia Sh 120,000 kwa mwaka.

Amesema gharama hizo zimewekwa ili kuwawezesha vijana wengi kupata fursa ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi bila kukwamishwa na gharama kubwa.

CPA Kasore amesema kupitia vyuo vyake, VETA imekuwa ikikuza ubunifu katika sekta mbalimbali kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wananchi pamoja na kurahisisha shughuli zao katika mazingira bora.

Amesema ubunifu huo ni sehemu ya juhudi za VETA kuhakikisha vijana wanapata ujuzi unaoendana na mahitaji ya sasa na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi, ajira na kujiajiri.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...