Kampuni ya Vodacom Tanzania inaendelea kuimarisha huduma za kifedha na mawasiliano kwa wananchi kupitia ushiriki wake katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nyamhongolo mkoani Mwanza. Katika maonesho hayo, watoa huduma wa kampuni hiyo wamekuwa wakitoa elimu na kusajili wananchi kwenye huduma mbalimbali, ikiwemo huduma ya Lipa.

Kupitia huduma ya M-Kulima, Vodacom inalenga kuwapatia wakulima suluhisho rahisi, salama na la uhakika la kupokea malipo yao wanapouza mazao. Huduma hii inalenga kuongeza uwazi na ufanisi katika miamala ya kifedha kwa wakulima, huku ikichangia kukuza uchumi wa sekta ya kilimo nchini. Vodacom inaendelea kujitolea kutoa huduma bunifu zitakazowawezesha wananchi, hasa wakulima, kunufaika zaidi na teknolojia ya kidijitali.


Mtoa huduma wa Vodacom Tanzania Catherine Masanja (kushoto) akimsajilia line ya Lipa mkazi wa Igoma Irene Ernest, kwenye maonesho ya Wakulima katika viwanja vya Nyamhongolo mkoani Mwanza, Kampuni hiyo iko katika maonesho ya Nanenane ikiwaelezea wananchi bidhaa na huduma mablimbali inazotoa ikiwamo M-Kulima huduma inayowapa wakulima njia rahisi na salama ya kulipwa mapato yao pindi wanapouza mazao mbalimbali.



Mtoa huduma wa Vodacom Tanzania, akiwaeleza wateja kuhusu Router kwenye maonesho ya Wakulima katika viwanja vya Nyamhongolo mkoani Mwanza.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...