WADAU wa Forodha wakiwemo Mawakala wa Forodha na Maafisa Forodha Mkoa wa Kigoma wamejengewa uwezo kuhusiana na mabadiliko yaliyofanywa na Serikali kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2026 pamoja na taratibu Forodha.
Elimu hiyo imelenga kuwawezesha
Wadau wa Forodha kuwa na uelewa wa pamoja juu ya Sheria, kanuni na taratibu za forodha na kuwawezesha kutimiza majukumu yao kwa ufanisi na kulipa kodi za Serikali kwa usahihi ili kurahisisha ufanyaji wa biashara na kukuza uchumi nchini.
Elimu hiyo imetolewa na Allan Maduhu, Afisa Forodha Mkuu na Hassan Minga, Afisa Mfawidhi Forodha-Dodoma ambao wamewataka wadau wa Forodha kufuata sheria na taratibu ili kuwawezesha kutekeleza sheria mpya ya Fedha ya mwaka 2026 ikiwemo kufahamu misamaha mbalimbali iliyotolewa na serikali kwa lengo la kuchochea sekta za uzalishaji pamoja na ukuaji wa viwanda nchini.
Misamaha iliyotolewa ni pamoja na msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye nyuzi za kutengenezea nyavu za uvuvi, nyavu za uvuvi zilizozalishwa na wazalishaji wa nyavu za uvuvi nchini pamoja na vifungashio vya maziwa kwa ajili ya kuchochea sekta ya maziwa nchini.
Aidha, Kaimu Meneja Msaidizi wa Forodha Mkoa wa Kigoma Mohamed Mnonda, amesema kulingana na shughuli za Forodha wamejipanga kutekeleza Sheria ya Fedha 2026 ili kuongeza uwajibikaji na ufanisi wa kiutendaji ili kuwezesha na kuboresha ufanyaji wa Biashara mkoani Kigoma.





.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...