Na Mwandishi Wetu

TAKRIBANI wiki moja tangu agizo la kuondoa Stendi za Mabasi mitaani lianze kutekelezwa Jijini Dar es Salaam, wadau mbalimbali wamedai kushangazwa na hatua hiyo na kuiomba Serikali kurejesha huduma hiyo ili kuwaondolea usumbufu wananchi.

Wamesema hatua hiyo inatokana na ukweli kuwa wananchi wameanza 'kuonja joto la jiwe' kutokana na umbali kati ya mahali kilipo Kituo cha Mabasi cha Magufuli na maeneo watokapo hali inayowafanya wapate wakati mgumu. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na njia mbalimbali, pamoja na mambo mengine wadau hao wamesema hakuna kingine kitakachowaondolea adha hiyo wananchi zaidi ya busara za viongozi pamoja watoa huduma na kwamba kwa namna ilivyo inaonesha kama kuna hali ya kutaka kukomoana.

Mkazi wa Kigamboni ambaye pia ni Mwandishi wa vitabu na mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kigamboni katika Uchaguzi wa Oktoba Mwaka jana kupitia CHAUMA Yericko Nyerere, amesema kama lengo la Serikali ni kurahisisha maisha ya wananchi basi inaonesha kuwa haijashauriwa vizuri  kuviondoa vituo vya mabasi mitaani.

Kupitia andiko lake katika akaunti yake ya  mtandao wa kijamii wa Instagram, amesema ikiwa Jiji la Dar es Salaam lina Wilaya tano (5) tena zikiwa maeneo ya mbalimbali na zote zikiwa na idadi kubwa ya watu, haiwezekani kutolea mfano wa Kituo Cha 'SGR' Bandari au Airport ukasema ndiyo mfano wa Stendi ya mabasi kuwa sehemu moja.

Amesema Dar es Salaam inayokadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya Milioni 7, wastani wa asilimia 84 ya wananchi wake hutegemea usafiri wa mabasi huku kwa siku ikikadiriwa kuwa takribani watu laki 2 wanaingia na kutoka kupitia usafiri huo Jijini humo hivyo ni ngumu wote kuwajaza sehemu moja.

"Kutoka Kata ya PembaMnazi, Wilaya ya Kigamboni hadi Stendi ya Magufuli ni kilomita 67, chukulia huyu mwananchi anataka kusafiri kwenda Mbeya huyu hawezi kutoka alfajiri akawahi basi pale Magufuli, atalazimika kusafiri siku moja kabla akalale Mbezi  Stendi ili asubuhi awahi basi na hii ni karbe ya 21 ya Sayansi na tekonolojia" amesema Nyerere.

Mdau mkubwa wa mitandao ya Kijamii Christopher Cyrilo,  ameenda mbali na kuhoji kuwa lipi lengo hasa la agizo hilo, je ni kuongeza mapato kwa Serikali kupitia stendi ya Magufuli au kuna sababu nyingine lakini kabla ya kuwatoa katika maeneo waliyokuwa wenye Mabasi hao walipata wapi vibali vya kutoa huduma maeneo hao.

" Je Ofisi hizo zilipata Usajili wa LATRA ? kama hazikujasiliwa Kuna adhabu  wamepewa na kama walisajiliwa je watalipwa fidia kwa usumbufu? " Amehoji Cyrilo kupitia andiko lake katika mtandao wa kijamii wa Facebook

Ameongeza kuwa endapo LATRA ilitoa Usajili alafu Mkuu wa Mkoa naye akatoa agizo lake kunaonesha kuna hali ya kutofautiana ndani Ofisi hizo mbili za Serikali huku akihoji ni faida zipi ambazo abiria wa mikoani wananufaika nazo kutokana na agizo hilo la Chalamila.

Amesisitiza kuwa anachoona yeye hatua ya wafanyabiashara wa mabasi kujenga Ofisi zao Shekilango, Chanika, Manzese, Magomeni, Kigamboni na kwingineko kulilenga kurahisisha huduma za usafiri kwa wateja wapo ili kuwaondolea hali ya usumbufu.  

Aidha  Chama Cha Wamiliki wa Mabasi nchini ( TABOA) kupitia kwa Katibu  wake Mkuu Priscus John Nimesema pamoja na agizo hilo wanachoiomba Serikali kuwaruhusu kwenda kushusha abiria wao katika maeneo mengine zilipo Ofisi zao mara baada ya kuingia na kushusha katika Kituo Cha Magufuli.

Amesema hawaoni tatizo kama mabasi yatapita Magufuli kushusha pamoja na kufanyiwa ukaguzi mbambali na taasisi za Serikali hususani Uhamiaji na zingine kIsha kwenda kushusha abiria maeneo mengine kwani kufanya hivyo pamoja na mambo mengine kutawaondolea Hali ya usumbufu abiria.

Hata hivyo wakati hayo yakiendelea kutokea imedaiwa kuwa zipo baadhi ya kampuni za Mabasi zimeamua kusitisha huduma zao za kusafirisha abiria na 'kupaki' mabasi yao kutokana na hali hiyo jambo lililopelekea baadhi ya watoa huduma wa Kampuni hizo kupata wakati mgumu kutokana na kukosa ajira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...