Na Nasra Ismail, Geita
Shirika la Arusha Society for the Protection of Animals (ASPA) kwa kushirikiana na Brooke East Africa limeendelea kutoa elimu kwa wafugaji na waendesha punda katika Kata ya Magenge, Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Hii imechangia kuboresha ustawi wa mnyama kazi huyo katika maeneo hayo.
Kupitia elimu wanayopatiwa na mashirika hayo, wamiliki na waendesha punda wameanza kuona faida ya kumtunza mnyama huyo ambaye sasa ameanza kuwaingizia kipato tofauti na awali.
Wananchi wamesema sasa wana elimu ya kumtunza punda na namna sahihi ya kumfungia mkokoteni. Hii imesaidia kumpunguzia mnyama huyo vidonda na mateso, tofauti na kipindi kilichopita kabla ya kupata elimu hiyo.
Afisa Mifugo wa Kata ya Magenge, George Sebastianamesema kupitia elimu inayotolewa na ASPA, kwa kipindi kirefu sasa punda wameanza kuzaliana. Hii inaonesha kuwa punda sasa wanapata ustawi na wanaishi vizuri.
Kwa upande wake, Afisa Elimu ya Ustawi wa Wanyama kutoka ASPA, Diana Msemo amesema mnyama kazi punda anahitaji utulivu wa hali ya juu ili aweze kufanya kazi zake za kiasili na kuongeza uwezekano wa kupata ujauzito na kuongeza kizazi chake.
Msemo amebainisha baadhi ya mambo yanayompa utulivu mnyama huyo ni pamoja na kupata muda wa kupumzika, kupewa matibabu ya mara kwa mara na kupunguziwa mizigo ambayo haimudu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...