Na Victor Masangu, Kibaha

Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwakomboa wanawake katika kujikwamua kiuchumi Azania bank imeamua kuja na mpango kabambe uliopewa jina la Fanikisha Mwanamke Hodari ambao utaweza kuwasaidia kupata mikopo yenye riba nafuu ambayo itawasaidia kiasi kikubwa kuendesha shughuli zao na kujiingizia kipato lengo ikiwa ni kuodokana na wimbi la umasikini na kujikwamua kiuchumi.

Hayo yamebainisha na Meneja wa Azania bank tawi la Kibaha mjini Anna Monyo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na baadhi ya wanawake kutoka kata mbali mbali za Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha kwa lengo la kuweza kuwapatia elimu na mafunzo mbali mbali yanayohusiana na fursa zilizopo ikiwa pamoja na jinsi ya kutumia mkopo ambao wanautoa wenye riba nafuu ya asilimia 1 kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Meneja huyo amebainisha kwamba lengo kubwa na mikakati ambayo wamejiwekea ni kuhakikisha kwamba wanamwezesha mwanamke kwa kumpatia mikopo ili aweze kupiga hatua na kusonga mbele zaidi na kutimiza ndoto zake alizonazo katika suala zima la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

"Tunashukuru sana kukutana na baadhi ya wanawake wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na kitu kikubwa ambacho tumekifanya ni kuweza kuwasogezea huduma yetu kwa ukaribu kwani tumeweza kufungua tawi letu la Azania bank hapa Kibaha na kwamba mtu anaweza kukopa kuanzia kiasi cha shulingi laki mbali hadi kiasi cha milioni 5 kulingana na uwezo wake alionao.

Meneja huyo amebainisha kwamba katika kutambua umuhimu wa wanawake wameamua kuja na akaunti hiyo maalumu ambayo itaweza kuwa ni mkombozi mkubwa ya kuwainua kiuchumi wanawake ambao ni wajasiriamali na kupitia akaunti hiyo wataweza kutimiza ndoto zao walizojiwekea.

Kadhalika ametoa wito kwa wanawake hao kuhakikisha wanajiunga katika vikundi mbali mbali vya ujasiriamali ili kuweza kupata fursa ya mikopo hiyo kwa urahisi na kwamba endapo wakiwa na kikundi wataweza kupatiwa mikopo hiyo ambayo itaweza kuwasaidia kuondokana na kuwa tegemezi na kuondokana na wimbi la umasikini.

Nao baadhi ya wanawake ambao wameweza kupata fursa ya kupatiwa elimu mbali mbali wameushukuru uongozi mzima wa Azania Bank tawi la Kibaha chini ya Meneja wake kwa kuweza kuona umuhimu mkubwa wa kuwatembelea na kuwapa mwenendo mzima wa elimu ambayo itaweza kuwasaidia katika suala zima la utunzaji wa fedha na kutimia vizuri fursa za mikopo ambayo inatolewa kwa riba nafuu ya kiwango cha asilimia 1 kwa mwezi mmoja.



Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...