Na MWANDISHI WETU


BALOZI wa Msumbiji nchini Tanzania, Ricardo Mtumbuida, amesema mataifa hayo yataendelea kuenzi, udugu, umoja na ushirikiano ulioasisiwa katika harakati za ukombozi wa mataifa hayo.

Amesema nchi za Tanzania na Msumbiji zinahistoria ya kipekee katika harakati hizo kwani Chama cha Ukombozi cha Msumbiji (FRELIMO) kiliasisiwa chini Tanzania .

Balozi Mtumbuida amryasema hayo leo Septemba 7,2026 Dar es Salaam, katika maadhimisho ya miaka 52 ya makubaliano ya Msumbiji na Ureno ya kumaliza vita yaliyosainia Lusaka, nchini Zambia mwaka 1974.

Ameeleza, vita ya ukombozi wa Msumbiji ilianza mwaka 1664 ambapo Septemba 7 mwaka 1974 Wareno wakatambua haki ya kufanya mapatano.

"Ndiyo maana sisi tunaita septemba 7 kila mwaka ni siku ya ushindi na ni kweli kwamba tulishinda vita hii kwani tulimshinda Mreno,"amesema Balozi Mtumbuida.

Amebainisha maadhimisho hayo ya miaka 52 ni muhimu hasa kwa jumuiya ya wananchi wa Msumbiji waishio hapa nchini .

"Tunapaswa kuwaambia historia watoto wetu, wajukuu na watu wote waliopo wakati huu kwani vita ya kukomboa Msumbiji ilianzia hapa Tanzania,"amesema.

Ameeleza Chama cha FRELIMO ambacho kimeongoza vita ya ukombozi wa Msumbiji, liliasisiwa hapa Tanzania.

"Kwa hiyo sisi jumuiya ya Wanamsumbiji tuishio Tanzania tunanafasi ya kipekee kukaa katika kitovu cha uhuru wetu,"ameeleza balozo huyo.

Amewataka wananchi wa Msumbiji waishio hapa nchini kuendelea kuenzi historia hiyo muhimu na kuwashirikisha watoto kujua historia hiyo muhimu.

"Nawapongeza wazazi walioleta watoto hapa na mimi nimekuwa nikieleza historia hii mara kwa mara, kuhusu umuhimu wa siku hii.,"amesema.

Mtumbuida alishukuru ushiriki wa Watanzania katika maadhimisho hayo hususan Kampuni ya Uhuru Publications Limited (UPL) wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo, Burudani na Uhuru ya Kijani .

"Tunashukuru kuona chombo hiki cha habari kinachomilikiwa na Chama Cha Mapindizi (CCM) kiko hapa. Hii yote nio kuendeleza mshikamano na ushirikiano wetu. Pia wapo wananchi wa Tanzania hapa,"ameeleza Mtumbuida.

Katika maadhimisho hayo, Balozi Mtumbuida, aliwaongoza wananchi wa Msumbiji waishio hapa nchini kuweka mashada ya maua katika kaburi ya mashujaa wa mapambano ya kupigania uhuru wa taifa hilo.

Makaburi hayo ni kaburi la maziko ya kwanza ya Rais wa wa FRELIMO, Dk. Eduardo Chivambo Mondlane, kaburi la aliyekuwa mke wa kwanza wa Rais wa Msumbiji, Samora Machel, Jozina Machel na shujaa mpigania uhuru wa taifa Francisco Manyanga.

Kwa upande wa Mondlane alizikwa kwa mara ya kwanza mnamo Februari 6, 1969, katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, baada ya kuuawa kwa bomu la kwenye bahasha Februari 3, 1969 ambapo baadaye mabaki ya mwili wake yalifukuliwa na kwenda kuzikwa nchini Msumbiji.

Mpigania uhuru wa Msumbiji Paul Matete Lekanone, alisema siku hiyo ya Septemba 7 kila mwaka ni kumbukumbu muhimu ya Ushindi Msumbiji baada ya mkutano wa makubaliano uliofanyika jijini Lusaka, nchini Zambia katika ya serikali ya Ureno na Msumbiji na kusaini makubalano hayo ya Uhuru wa Msumjini ulipatikana Juni 25, 1975.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...