CHAANI, ZANZIBAR


NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndg. Abdi Mahmoud Abdi, amesema CCM inaandaa mkakati imara wa kuimarisha uhai wa chama hicho ili kiendelee kudumu na kutoa mchango mkubwa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Ndg. Abdi amesema hayo leo, Septemba 5, 2026, wakati akizungumza na viongozi pamoja na wajumbe wa Kamati za Siasa za Mkoa na Wilaya katika Jimbo la Chaani, Zanzibar.

Amepongeza hatua zinazochukuliwa na viongozi wa Jimbo la Chaani katika kuimarisha maendeleo ya chama na wananchi, akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha rasilimali za chama zinasimamiwa kwa ufanisi na kutumika kwa manufaa ya chama, wananchi na Taifa.

Amesema moja ya malengo ya ziara yake ni kukagua mali za CCM na kujionea namna zinavyosimamiwa na kuendelezwa ili ziweze kutoa tija kwa chama na wananchi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Chaani, Ndg. Ayoub Mohammed Mahmoud, amesema jimbo hilo lina mali mbalimbali zinazoweza kuchangia maendeleo ya CCM, ikiwemo fremu za maduka pamoja na miradi mingine ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.

Amesema viongozi wanaendelea na mpango wa ujenzi wa jengo la CCM litakaloendana na hadhi ya chama, huku likiwa na huduma mbalimbali pamoja na ukumbi mkubwa utakaotumika kwa shughuli za chama na shughuli za kijamii.

Hata hivyo, Mbunge huyo ametaja ukosefu wa miundombinu ya barabara za kisasa kuwa miongoni mwa changamoto zinazolikabili Jimbo la Chaani, akisema hali hiyo inarudisha nyuma kasi ya maendeleo katika baadhi ya maeneo.

Akitoa ufafanuzi kuhusu changamoto hizo, Ndg. Abdi amesema amezipokea na atazifanyia kazi kwa lengo la kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati.

Awali, mara baada ya kuwasili Jimboni Chaani, Ndg. Abdi alipokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za jimbo hilo, ikiwemo miradi ya maendeleo ya chama na jitihada za kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Taarifa hiyo pia imeeleza hatua zinazochukuliwa katika kuwawezesha vijana kupata elimu, kuboresha huduma za michezo pamoja na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...