Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndugu Abdi Mahamoud Abdi, amesema CCM imeridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya Chama kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa katika sekta ya elimu nchini.

Ndugu Abdi ameyasema hayo wakati akiendelea na ziara ya kukagua uhai wa Chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Donge, ambapo alipata fursa ya kukagua ujenzi wa dahalia ya wanafunzi wa kike katika Skuli ya Donge.

Amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa dahalia hiyo, akieleza kuwa kukamilika kwake kutaimarisha mazingira ya kujifunzia na huduma za elimu kwa wanafunzi wa kike katika eneo hilo.

Aidha, Ndugu Abdi amesema viongozi wakuu wa kitaifa, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, wameendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha huduma za jamii, kunufaisha wananchi na kukuza uchumi wa nchi.

Amewapongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (WEMA) kwa usimamizi wa miradi mbalimbali ya elimu, akisema juhudi hizo zitasaidia kupunguza changamoto zinazoikabili sekta hiyo na kuboresha huduma za elimu visiwani Zanzibar.

Kwa upande wao, viongozi wa Jimbo la Donge wamesema eneo hilo limeendelea kupiga hatua za kimaendeleo kutokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta za kijamii na kiuchumi.

Akitoa taarifa ya kitaalamu, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ndg. Mwanahamis Adam, amesema kukamilika kwa ujenzi wa dahalia hiyo kutasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na huduma za elimu kwa wanafunzi wa kike Zanzibar.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...