Na Mwandishi wetu, Simanjiro
MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Fakii Raphael Lulandala ameingilia kati mgogoro wa ardhi kwa kuagiza waliovamia eneo la shule ya serikali ya Saniniu Laizer ya kijiji cha Naepo Kata ya Naisinyai kusitisha ujenzi wake.
DC Lulandala ameagiza waliovamia eneo hilo kusitisha shughuli za ujenzi na ndani ya siku 14 tafsiri ya mipaka ifanywe na wataalam wa ardhi na kuweka alama ya mipaka eneo la shule hiyo ya Saniniu Laizer.
Hata hivyo, Lulandala ameagiza uhakiki wa eneo la ekari 48 la mipaka ya shule hiyo ufanyike upya kwa usimamizi wa wataalamu wa ardhi na apewe taarifa baada ya siku saba.
Amewaagiza polisi na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) kuwahoji ofisa mtendaji wa kata hiyo Valentine Tesha, Mwenyekiti wa kijiji hicho Elias Abraham na aliyejenga nyumba eneo hilo Stephen Mollel.
"Haiwezekani mtendaji wa kata Tesha na Mwenyekiti wa kijiji, nyumba ijengwe na kupauliwa ninyi mnaona tuu bila kuchukua hatua, polisi na Takukuru wahojini hawa viongozi kwa nini waliruhusu," amesema DC Lulandala.
Mchimbaji maarufu wa madini ya Tanzanite, bilionea Saniniu Laizer ambaye alijenga shule hiyo na kuikabidhi serikali amepongeza hatua iliyochukuliwa na DC Lulandala.
Diwani wa kata ya Naisinyai, Taiko Kurian amesema eneo hilo lilikuwa mali ya kijiji na likatengwa ekari 48 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ya awali na msingi ya serikali.
Mmoja kati ya watu wanaodaiwa kujenga nyumba eneo hilo Stephen John Mollel amekiri kupewa barua mbili tofauti za kusimamisha ujenzi wake ila akaendelea kujenga.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...