Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, imezindua Kamati ya Ushauri wa Kisheria ngazi ya Mkoa na Wilaya katika Mkoa wa Katavi. Uzinduzi huo umefanyika tarehe 8 Septemba, 2026 na kufuatiwa na kliniki ya Sheria bila malipo iliyoanza tarehe 7 Septemba, 2026 katika Viwanja vya Azimio Mpanda .

Uzinduzi wa Kamati za Ushauri wa Kisheria na Kliniki ya Kisheria bila malipo, ni dhamira ya dhati ya Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kutatua migogoro, kutoa ushauri wa Kisheria kwa wananchi na elimu ya Kisheria bila malipo.

Akizungumza katika hotuba yake ya Uzinduzi, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Jamila Yusuph, ameeleza kuwa jukumu la kutatua migogoro katika maisha ya watanzania sio la Serikali pekee ni jukumu la wadau wote wa maendeleo.

Mhe. Mkuu wa Wilaya amekuwa mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko katika Uzinduzi wa Kamati za Kudumu za Ushauri wa Kisheria ngazi ya Mkoa na Wilaya zimezinduliwa mkoani Katavi, tarehe 8 Septemba , 2026, katika Viwanja vya Azimio, Mpanda.

Akizungumza katika hafla hiyo, amesisitiza umuhimu wa wananchi kutumia fursa zinazotolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Kamati hizo pamoja na Kliniki ya Sheria ili kupata elimu, ushauri na ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria.

Akitoa shukrani zake Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari, amesema kuwa kitendo cha kusogeza huduma ya ushauri wa kisheria kwa wananchi wa mkoa wa Katavi zinaenda kutatua changamoto walizonazo wananchi za kisheria.

“Namshukuru Mhe. Hamza Johari, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Ofisi yake na Kamati ya kudumu ya Ushauri wa Kisheria ya Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na Ofisi yangu, kuweza kufanikisha sherehe hii ya Uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Kisheria na Kliniki ya Sheria bila Malipo Mkoa wa Katavi.” Amesema Mhe. Jamila Yusuph.






Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...