Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MANISPAA ya Kibaha imeweka mpango wa kujenga ofisi za walimu za kisasa katika kila shule, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha mazingira ya kazi na kupunguza changamoto ya ukosefu wa ofisi zinazowakabili walimu.
Meya wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Nicas Mawazo, ameyasema hayo wakati akizungumza na wazazi, walezi, wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi Kanesa, Kata ya Kongowe, ambapo amesema ujenzi huo unalenga kuwawezesha walimu kufanya kazi katika mazingira salama na bora.
Dkt. Nicas amesema Manispaa itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo pamoja na wazazi katika kutatua changamoto za miundombinu ya elimu, akieleza kuwa tayari imeanza kuchukua hatua katika baadhi ya maeneo, ikiwemo upatikanaji wa madawati.
Kuhusu changamoto ya ukosefu wa uzio katika Shule ya Msingi Kanesa, Dkt. Nicas amewataka wakuu wa shule kuhakikisha maeneo ya taasisi za umma, ikiwemo shule, yanarasimishwa na kupatiwa hati ifikapo Februari 2027.
Amesema urasimishaji wa maeneo hayo utasaidia kulinda mali na maeneo ya taasisi za umma dhidi ya uvamizi na umegaji wa maeneo hayo, akieleza kuwa Manispaa ilianza zoezi hilo mwaka 2025 na gharama ya urasimishaji ni Shilingi 130,000.
Aidha, Dkt. Nicas amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao na kuwa tayari kushindana katika soko la ajira, huku akiwataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha watoto wanaendelea na elimu ya sekondari.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Africans Co. Ltd, Hafidh, amesema kampuni hiyo itapeleka samani katika Shule ya Msingi Kanesa, zikiwemo kwa ajili ya ofisi za walimu, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kanesa, Jordan Ngairo, amesema changamoto kubwa inayoikabili shule hiyo ni ukosefu wa uzio, hali ambayo amesema inaweka hatarini usalama wa wanafunzi pamoja na mali za shule.
Amesema shule hiyo pia inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa umeme, maji, vyoo vya walimu na darasa la awali, pamoja na upungufu wa samani, ambapo inahitaji viti na meza 96 kwa ajili ya ofisi za walimu.
Shule ya Msingi Kanesa imefanya mahafali yake ya tatu ikiwa na jumla ya wanafunzi 1,204, ambapo wanafunzi 129 wamehitimu.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...