Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amewasilisha taarifa kuhusu mafunzo ya kuongeza uelewa wa itikadi ya CCM, ujenzi wa Chama na kuongeza wanachama wapya, yaliyohitimishwa leo Septemba 30, 2026, katika Chuo cha Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Tunguu, Zanzibar.
Mafunzo hayo ya awamu ya pili yamehitimishwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Kihongosi amesema usaili wa makada waliohudhuria mafunzo hayo ulizingatia uelewa wa historia, muundo, misingi na itikadi ya CCM, uwezo wa kujenga na kuwasilisha hoja, mbinu za ufundishaji, maadili na nidhamu, pamoja na uwezo wa kuendeleza elimu ya Chama.
Amesema mfumo huo wa usaili umewezesha kuweka viwango vinavyofanana vya uteuzi kabla ya makada hao kuanza mafunzo.
Kwa mujibu wa Kihongosi, mchakato huo wa usaili umekamilisha hatua muhimu ya udhibiti wa ubora kwa kuunganisha viwango vya uteuzi katika mikoa 32 na wilaya 168.
Amesema mafunzo hayo yamejikita katika maeneo mbalimbali, yakiwemo muundo na historia ya CCM, misingi na itikadi ya Chama, maadili katika itikadi na falsafa ya CCM, ujenzi wa makada, ujenzi upya wa imani ya wanachama na wananchi, pamoja na uwezo wa kujenga hoja.
Aidha, amesema mafunzo hayo yamezingatia matumizi ya mazingira ya kidijitali katika utoaji wa elimu na mawasiliano ya kisiasa, hatua inayolenga kuwawezesha makada kuendana na mabadiliko ya teknolojia na mazingira ya sasa ya mawasiliano.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...