▪️Ni cha Kampuni ya Madini ya Shenghe ambacho ujenzi wake umeanza
▪️Madin ya mchanga mzito kutoka nchi mbalimbali Afrika kuchakatwa Pangani,Tanga
▪️Waziri Mavunde apongeza hatua ya kuifanya Tanzania kitovu cha uongezaji thamani madini Afrika
▪️Awataka wawekezaji kukamilisha ujenzi wa kiwanda mapema
▪️Rais Samia apongezwa kwa mazingira rafiki ya uwekezaji
Chengdu,China
Kampuni ya Shenghe Resources ya China imeanza ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata madini madini ya mchanga mzito wa baharini (๐๐๐๐ซ๐ฎ ๐๐๐ฃ๐๐ง๐๐ก ๐๐๐ฃ๐๐จ) katika eneo la Tajiri,Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga ambapo kampuni hii inatekeleza mradi mkubwa wa uchimbaji wa madini tembo.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Shenghe Ndg. Xie Bing wakati wa ziara ya Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde kutembelea na kujionea shughuli mbalimbali za uongezaji thamani madini zinazofanywa kampuni hiyo.
Akizungumza katika ziara hiyo Ndg. Bing amesema kwa Bara la Afrika wana miradi ya madini hayo katika nchi za Msumbiji, Afrika ya Kusini na Madagascar lakini wameichagua Tanzania kuwa ndio kitovu cha uchakataji madini hayo barani Afrika na sasa wameanza ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata madini hayo(๐๐๐ฃ๐๐ง๐๐ก ๐๐๐ฅ๐๐ง๐๐ฉ๐๐ค๐ฃ ๐๐ก๐๐ฃ๐ฉ) wilayani Pangani,Tanga na kuahidi kukamilisha ndani ya muda mfupi ujao ambapo malighafi kutoka nchi nyingine za Afrika zitaletwa Tanzania kwa ajili ya uchakataji wake na kuongezea thamani.
Aidha,Ndg. Bing ameipongeza Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Mh. Rais Samia S. Hassan kwa mazingira rafiki ya uwekezaji ambayo yamewavutia kuja kuwekeza Tanzania.
Akizungumza katika ziara hiyo,Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amepongeza maamuzi hayo makubwa ya Kampuni ya Shenghe ambayo yanaendana na sera ya Madini na Sheria ya Madini ya takwa la uongezaji thamani madini nchini na kusema hatua hiyo itachochea upatikanaji wa Ajira,Kuongezeka kwa mapato na kukua kwa teknolojia katika eneo la uchakataji madini.
Aidha Waziri Mavunde ameitaka Kampuni ya Shenghe kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa kiwanda hicho kwa wakati na pia inamalizia malipo ya fidia kwa maeneo machache yaliyobaki.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...