Na MWANDISHI WETU, Zanzibar

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Abdi Mahamoud Abdi, amesema mafunzo ya uongozi ni muhimu katika kuwawezesha viongozi na wanachama wa chama hicho kuwa wazalendo, pamoja na kuzingatia na kutekeleza sera, kanuni na taratibu za CCM.

Abdi ameyasema hayo leo, Septemba 26, 2026, wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya Itikadi, Uenezi na kuongeza wanachama wapya wa CCM kwa awamu ya pili, yaliyofanyika Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema CCM imekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo ya uongozi kwa wanachama wake kwa lengo la kuwaongezea uelewa na uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi na taratibu za chama.

Amesema elimu inayotolewa kwa viongozi na wanachama kupitia mafunzo hayo itasaidia kukiimarisha CCM na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za chama, pamoja na kuchangia juhudi za kuleta maendeleo kwa ujumla.

Aidha, Abdi amewataka washiriki kutumia fursa hiyo kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuongeza uelewa kuhusu Itikadi, Uenezi na misingi ya CCM ili elimu watakayoipata iweze kutumika ipasavyo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Amesisitiza kuwa uelewa mzuri wa misingi na taratibu za chama ni muhimu kwa viongozi na wanachama katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa kuzingatia malengo ya CCM.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...