Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratias Ndejembi, amewasili jijini New York, Marekani, kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81).
Mhe. Ndejembi amewasili nchini Marekani kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy, ambapo amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsie Kanza, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York, Mhe. Togolani Mavura, pamoja na maafisa mbalimbali.
Mkutano huo wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unawakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali pamoja na viongozi mbalimbali kutoka mataifa duniani kujadili masuala muhimu ya kimataifa, yakiwemo uchumi, siasa, mazingira na haki za binadamu.
Mkutano wa mwaka huu unaongozwa na kaulimbiu “Kurudisha Imani, Kusimamia Mabadiliko: Umoja wa Mataifa Unaohudumia Wote” (Restoring Trust, Managing Transformation: A United Nations That Delivers for All).
Kaulimbiu hiyo inalenga kuhimiza kujenga upya uaminifu na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na mabadiliko makubwa yanayoendelea duniani, ikiwemo maendeleo ya kasi ya teknolojia ya akili unde (AI).
Katika ziara hiyo, Mhe. Ndejembi anatarajiwa kuhutubia Kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kushiriki katika shughuli mbalimbali za mkutano huo, zikiwemo Mjadala Mkuu (General Debate), mikutano ya pembezoni pamoja na mikutano ya pande mbili (Bilateral Meetings) na viongozi na wawakilishi wa mataifa mbalimbali.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...