Mashindano ya Kombe la Faru yameanza kwa kishindo kwa kata ya Ngorongoro kuitandika kata ya Kakesio magoli 6-0 katika mchezo uliopita kwenye viwanja vya shule ya msingi Makao wilayani Ngorongoro.
Katika mtanange huo timu ya kata ya Ngorongoro ilionesha mchezo wa viwango vya kimataifa huku ikihakikisha inafika katika lango la kata ya Kakesio kila baada ya dakika tano.
Timu ya kata ya Ngorongoro iliweza kupata magoli katika kipindi cha kwanza na cha pili ambapo mchezo huo ulichagizwa na ushangiliaji mkubwa kutoka kwa mashabiki wa kata ya Ngorongoro.
Mashindano hayo yanafadhiliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambapo mshindi pamoja na mambo mengine atapata nafasi ya kushuhudia dabi ya Simba na Yanga.



.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...