Uongozi wa Kata ya Mnadani umeanza kuchukua hatua za tahadhari kwa kukagua maeneo hatarishi yanayoweza kuathiriwa na mvua za El Nino.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Diwani wa Kata ya Mnadani, Mugendi Kerenge, alisema kuwa ukaguzi huo unafanyika kwa kushirikiana na Kamati ya Maendeleo ya Kata pamoja na viongozi wa Kanda Namba Sita, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Nino.
“Tumeanza kukagua maeneo ambayo tunaona yanaweza kuwa na changamoto wakati wa mvua, hasa sehemu zinazotuamisha maji na mitaro ambayo inahitaji kufunguliwa na kusafishwa,” alisema Kerenge.
Aidha aliongeza kuwa ufunguaji na usafishaji wa mitaro ni miongoni mwa hatua muhimu zinazotekelezwa ili kuhakikisha maji yanapata njia ya kupita na hivyo kupunguza uwezekano wa mafuriko na madhara mengine.
Aliwataka wananchi kushirikiana na viongozi kwa kuhakikisha mitaro na njia za maji zinakuwa wazi, pamoja na kutoa taarifa kuhusu maeneo yanayoweza kuwa hatarishi ili hatua zichukuliwe kwa wakati kwani zoezi la ukaguzi ni endelevu
Ziara hiyo ilishirikisha viongozi wa Kanda Namba Sita kubaini maeneo yanayoweza kukumbwa na changamoto za maji, ikiwemo maeneo yanayotuamisha maji pamoja na mitaro inayohitaji kufunguliwa na kusafishwa ili kurahisisha mtiririko wa maji wakati wa mvua.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...