Na Mwandishi wetu, Babati
NAIBU waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Ndege amechangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa shule ya sekondari Mbugwe Wilayani Babati Mkoani Manyara.
Pamoja na hayo Naibu Waziri Ndege ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Manyara, amekabidhi shilingi milioni moja kwa ajili ya motisha kwa walimu wa shule hiyo.
Ametoa mifuko hiyo ya saruji na fedha hizo kwenye mahafali ya wahitimu wa kidato cha nne wa shule hiyo ya sekondari Mbugwe.
Pia, amekabidhi sare za michezo kwa wanafunzi wa shule hiyo kwa ajili ya kushiriki michezo kipindi cha mapumziko ya masomo.
Akizungumza kwenye mahafali hayo Naibu Waziri Regina amewaasa wanafunzi hao wahitimu kuhakikisha wanajipanga ipasavyo kwenye mitihani ya kuhitimu.
Naibu Waziri Regina amesema kwa wanafunzi hao walipofikia ni mwanzo tu wa safari yao ya kimasomo hivyo wazidi kusoma kwa bidii kwa kipindi kifupi kilichobaki kabla ya kufanya mitihani.
"Endeleeni kuwa na tabia njema kwenye kipindi chote mtakapokuwa nyumbani kwenu wakati mkisubiria matoleo mara baada ya kufanya mitihani yenu," amesema Naibu Waziri Regina.
Hata hivyo, viongozi wa shule ya sekondari Mbugwe wamempongeza na kumshukuru Naibu Waziri Regina kwa moyo wa kujitolea na kuchangia mifuko hiyo 100 ya saruji na fedha shilingi milioni moja.
Naibu Waziri Regina amembatana na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Manyara, Fatuma Tsea, Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa Janes Darabe ambaye pia aliwahi kufundisha kwenye shule hiyo na Diwani wa Kata ya Kisangaji Adam Ipingika.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...