Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndg. Abdi Mahamoud Abdi, amewatembelea na kuwajulia hali wazee wa chama, akiwemo Balozi wa CCM wa Shina Namba 21, Ndg. Mtumwa Ali Ndevu, nyumbani kwake Mkwajuni, Zanzibar.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Ndg. Abdi amesema ni muhimu kwa viongozi na wanachama wa CCM kuendelea kuwathamini, kuwaheshimu na kuwajali wazee ambao wamekuwa sehemu muhimu ya historia, ujenzi na mafanikio ya Chama Cha Mapinduzi.
Amesema CCM inatambua mchango mkubwa wa wazee wake katika kulinda misingi, misimamo na maadili ya chama, hivyo viongozi na wanachama wana wajibu wa kuendelea kuwa karibu nao na kujifunza kutokana na uzoefu wao.
Kwa upande wake, Ndg. Mtumwa Ali Ndevu amemshukuru Ndg. Abdi kwa kumtembelea na kumjulia hali, akisema kitendo hicho ni ishara ya upendo, heshima na mshikamano uliopo ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za viongozi wa CCM Zanzibar kuendelea kuwa karibu na wanachama, viongozi wastaafu na wazee wa chama, kwa lengo la kuimarisha mshikamano, kuhifadhi historia ya chama na kuendeleza misingi ya Chama Cha Mapinduzi.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...