Iringa, Tanzania — Septemba 21, 2026

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Abdalla Hamid (MCC), amewataka viongozi wa CCM na Serikali kutimiza ipasavyo wajibu wao ili kutekeleza nia njema ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha kila mwananchi anaishi kwa matumaini na tabasamu.

Rabia ameyasema hayo leo, Septemba 21, 2026, wakati akiendelea na shughuli zake mkoani Iringa, ambapo amepokelewa rasmi katika Ofisi za CCM Mkoa wa Iringa na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo kutembelea vikundi vya wajasiriamali na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi.

Katika ziara hiyo, Rabia amekutana na kuzungumza na makundi mbalimbali ya wananchi, yakiwemo viongozi wa dini, wazee, machifu, wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, mafundi gereji, mafundi ujenzi, wanamichezo, wavuvi, wanafunzi wa vyuo, walimu, machinga, mama na baba lishe, watu wenye mahitaji maalum, wajane na wagane.

Makundi mengine aliyokutana nayo ni vyama vya ushirika, maafisa usafirishaji pamoja na vikundi mbalimbali vya ujasiriamali, huku akisikiliza changamoto zao na kutoa maelekezo kwa maeneo yanayohitaji hatua za Serikali na Chama.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...