Mkuu wa wilaya ya Kibiti Mhe. Kanali Joseph Kolombo ameipongeza Mamlaka ya Mpato Tanzania (TRA) kwa kuja na mfumo wa kutoa risiti za kielektroniki jambo ambalo linaokoa gharama za walipakodi katika kutimiza wajibu wao wa kikodi na kusema kuwa kila mtu awe balozi wa kuhamasisha matumizi ya risiti za kielektroniki

Ameyasema hayo alipotembelea banda la TRA katika maonesho ya Mafia Festival 2026 yanayofanyika katika viwanja vya Utende wilaya ya Mafia mkoani Pwani leo tarehe 25 Septemba, 2026. Mhe. Kolombo amesema walipakodi sasa wanaokoa gharama kwa kutoa risiti kupitia mfumo wa IDRAS jambo linalochochea ulipaji kodi wa hiari.

“Mfumo wa kutoa risiti sasa umerahisishwa zaidi hivyo utachochea ulipaji kodi wa hiari na sote tuwe mabalozi wa kuhamasisha matumizi sahihi ya risiti za kielektroniki” amesema Mhe. Kolombo.

Kwa upande wake Afisa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wa TRA Bi. Yusta Kaunda amesema TRA imeshiriki maonesho ya Mafia Festival 2026 na huduma mbali mbali za kodi zinatolewa katika banda la TRA kama vile; namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN), elimu ya uwasilishaji wa ritani za kodi, elimu kuhusu forodha, leseni za udereva, mfumo na mashine za kielektroniki za kuto risiti EFD/VFD, limu ya matumizi ya stempu za kielekroniki za kodi (ETS), elimu ya kodi katika utalii na uwekezaji na elimu ya kutumia mfumo wa IDRAS.

Aidha Bi. Yusta amewakumbusha wafanyabiashara kulipa kodi ya mapato awamu ya tatu kabla au mnamo tarehe 30 Septemba 2026.











Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...