Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) imeibuka mshindi wa kwanza na kutunukiwa Tuzo katika kipengele cha Shirika la Umma la Kibiashara lililofanya vizuri zaidi katika Menejimenti ya Rasilimali-Fedha, kupunguza matumizi na kuongeza ufanisi katika urejeshaji wa Mtaji.

Tuzo hiyo imetolewa leo wakati wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum 2026), kilichofanyika katika Ukumbi wa Arusha International Conference Centre (AICC), Arusha.
Makamu wa Rais, Mhe. Deo Ndejembi, ametoa pongezi kwa Tanga UWASA kwa kutambuliwa kwa utendaji wake, akisisitiza umuhimu wa Taasisi na Mashirika ya Umma kuendelea kuimarisha usimamizi wa rasilimali, kuongeza ufanisi na kuhakikisha yanatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.
Mafanikio hayo yanaendelea kuonesha umuhimu wa usimamizi bora wa rasilimali katika Taasisi na Mashirika ya Umma, hususan katika kuimarisha ufanisi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...