Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano la Sita la Jumuiya ya Taasisi za Mitaala Afrika (African Curriculum Association – ACA), litakalofanyika kuanzia Septemba 22 hadi 25, 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika kongamano hilo la siku nne anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratias John Ndejembi, ambaye anatarajiwa kuambatana na viongozi mbalimbali wa kitaifa pamoja na wawakilishi wa mashirika ya ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba, amesema TET kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Zanzibar (TEZ), imepewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa kongamano hilo litakalowakutanisha wataalamu na taasisi zinazohusika na ubunifu, uandaaji na uboreshaji wa mitaala barani Afrika.
Amesema kongamano hilo litatoa fursa kwa washiriki kubadilishana maarifa, matokeo ya tafiti, uzoefu na ubunifu kuhusu mabadiliko ya mitaala na mifumo ya elimu, kwa kuzingatia mahitaji ya sasa na ya baadaye ya Afrika na dunia kwa ujumla.
Dkt. Komba amesema Kongamano la ACA 2026 pia litatoa fursa kwa nchi nyingine kujifunza kutoka Tanzania na kushirikishana uzoefu kuhusu mageuzi ya mitaala yaliyofanyika nchini na kuanza kutekelezwa kuanzia Januari 2024.
“Kongamano hili linaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika na Lengo la Nne la Maendeleo Endelevu (SDG 4), ambazo zinasisitiza umuhimu wa kutoa elimu bora inayolenga kujenga wahitimu wenye ujuzi na uwezo wa kutumia ujuzi wao kutatua changamoto katika jamii zao,” amesema Dkt. Komba.
Amesema Tanzania imekuwa ikishiriki katika makongamano ya ACA yaliyofanyika katika nchi mbalimbali za Afrika, hivyo kuwa mwenyeji wa kongamano la mwaka huu ni fursa muhimu kwa nchi kuonesha mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu.
Kwa mujibu wa Dkt. Komba, mafanikio hayo ni pamoja na maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023, pamoja na maboresho ya mifumo ya elimu na mitaala.
Amesema kongamano hilo pia litaiwezesha Tanzania kubadilishana uzoefu na kujifunza kutoka nchi nyingine, huku ikichangia katika mwelekeo na maendeleo ya elimu barani Afrika.
Washiriki wa kongamano hilo wanatarajiwa kuwa waandaaji na waendelezaji wa mitaala, watafiti wa elimu, wataalamu na wadau wa mitaala na elimu kwa ujumla kutoka sekta ya umma na binafsi, watunga sera, washirika wa maendeleo na watekelezaji wa mitaala, wakiwemo walimu, wakufunzi, wahadhiri pamoja na wanafunzi wa shahada za uzamili na uzamivu katika masuala ya elimu kutoka Tanzania, Afrika na maeneo mengine duniani.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...