Na Janeth Raphael - MichuziTv
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kuanza kwa Awamu ya Pili ya udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2026/2027, hatua inayowapa fursa nyingine waombaji ambao hawakuweza kuwasilisha maombi au hawakupata nafasi ya kudahiliwa katika Awamu ya Kwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa, amesema Awamu ya Pili ya udahili imeanza Septemba 8 na itaendelea hadi Septemba 21, 2026, huku akiwataka waombaji kutumia fursa hiyo kutuma maombi katika vyuo na programu wanazozipendelea.
Prof. Kihampa amesema kukamilika kwa Awamu ya Kwanza kumebainisha kuwa jumla ya waombaji 149,645 waliwasilisha maombi ya kujiunga na Shahada ya Kwanza katika vyuo 93 vilivyoidhinishwa kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2026/2027, ambapo waombaji 117,334, sawa na asilimia 78.4 ya waombaji wote, wamepata udahili katika vyuo walivyoomba.
Amesema idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka baada ya kukamilika kwa Awamu ya Pili, ambayo imefunguliwa kwa waombaji ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kutuma maombi au hawakupata nafasi katika Awamu ya Kwanza.
Kwa mwaka wa masomo 2026/2027, TCU imeeleza kuwa kuna jumla ya programu 1,019 za Shahada ya Kwanza zinazotolewa na vyuo vilivyoidhinishwa, ikiwa ni ongezeko la programu 125 kutoka programu 894 zilizokuwepo mwaka wa masomo 2025/2026.
Aidha, nafasi za udahili zimeongezeka kutoka 205,652 mwaka uliopita hadi 227,555 mwaka huu, sawa na ongezeko la nafasi 21,903 au asilimia 10.7.
Katika hatua nyingine, waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja wametakiwa kuhakikisha wanathibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia Septemba 8 hadi 21, 2026. Uthibitisho huo utafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa waombaji kupitia ujumbe mfupi wa simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili.
Prof. Kihampa amesema waombaji ambao hawajapokea namba hiyo kwa wakati wanapaswa kuingia katika mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa tena ujumbe wenye namba maalum ya siri ili waweze kukamilisha uthibitisho wa udahili.
Tume imesisitiza kuwa uthibitisho wa udahili unatakiwa kufanyika kupitia akaunti ambayo mwombaji alitumia wakati wa kuwasilisha maombi yake, huku orodha ya waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja ikipatikana kupitia tovuti rasmi ya TCU.
Wakati huo huo, TCU imevielekeza vyuo vya elimu ya juu nchini kutangaza programu ambazo bado zina nafasi za udahili ili kuwawezesha waombaji kupata taarifa sahihi na kutumia fursa hiyo katika Awamu ya Pili. Waombaji na vyuo pia wametakiwa kuzingatia kalenda, miongozo na taratibu za udahili wa Awamu ya Pili zilizowekwa na TCU.
Kwa upande wa waombaji watakaokutana na changamoto katika masuala ya udahili au uthibitisho wa nafasi zao, TCU imewataka kuwasiliana moja kwa moja na vyuo husika, huku vyuo vikielekezwa kupokea taarifa hizo na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa na Tume.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...