Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) umeeleza kuwa, umedhamiria kuendelea kuboresha utoaji huduma kwa watalii kwa njia za kisasa kupitia matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano ili kuongeza ufanisi na kasi ya utendaji kazi na ukusanyaji wa mapato.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi anayesimamia huduma za Utalii na Masoko Mariam Kobelo ameeleza kuwa lengo la kufanya kazi kidigitali ni kuhakikisha kuwa watoa huduma katika sekta ya utalii wanatumia muda mfupi kuingia na kutoka ndani ya hifadhi pamoja na kuhakikisha maduhuli ya serikali yanakusanywa kikamilifu na kuimarisha usalama wa hifadhi na rasilimali zilizopo.
“Siku mbili zilizopita tumekuwa na changamoto ndogo ndogo katika lango kuu la Ladoure ,tunaendelea kuzitatua kwa ushirikiano mkubwa na wadau wetu”,amesema bi.Kobelo.
Amewashukuru waongoza watalii wote na wadau katika sekta hiyo kwa kuonesha ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha maboresho hayo.
Ameongeza kuwa mteja yeyote atakayekutana na changamoto za kiutendaji katika kipindi hiki ni vema akawasiliana na maafisa wa mamlaka hiyo ambao wapo katika lango hilo na maeneo mengine na watasaidiwa ili waweze kuendelea na safari zao kwa muda kama walivyopanga.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika mwelekeo wa utendaji wake mpya imedhamiria kuimarisha shughuli zake za kutoa huduma bora kwa watalii katika viwango vya kimataifa na kuendelea kuimarisha dawati la huduma na ukarimu kwa wateja.

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...