Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mulembwa Munaku, na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Asha Dachi, wamesaini mkataba wa kiutendaji baina ya taasisi hizo.

Utiaji saini wa mkataba huo umefanyika leo, Septemba 7, 2026, katika Ofisi za TBC, Mikocheni, jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF.

Mkataba huo unalenga kuimarisha ushirikiano na mahusiano ya kiutendaji kati ya UCSAF na TBC, pamoja na kuweka msingi wa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za pamoja kwa manufaa ya taasisi hizo na wananchi.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Asha Dachi, amesema UCSAF umekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha shughuli za kiutendaji za TBC, hususan kupitia uwezeshaji wa vifaa na huduma muhimu.

Amesema uwezeshaji huo umekuwa chachu ya kuboresha usikivu wa redio na muonekano wa televisheni wa TBC, hatua inayochangia kuongeza ufanisi wa huduma za utangazaji kwa wananchi.

Dachi amesema UCSAF pia imekuwa na nafasi muhimu katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi katika maeneo ya vijijini na maeneo mengine ambayo hayapati huduma za kutosha.

Ameongeza kuwa baadhi ya vituo vilivyowezeshwa na UCSAF ni Redio Jamii Dodoma na Redio Jamii Arusha.

Dachi ameyasema hayo leo, Septemba 7, 2026, wakati wa ziara ya Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF katika Ofisi za TBC, Mikocheni, jijini Dar es Salaam.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...