Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

WATU nane wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa baada ya gari la abiria aina ya Toyota Coaster kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania katika eneo la Chumbi, Kata ya Chumbi, Tarafa ya Mohoro wilayani Rufiji mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rufiji, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Protas Mutayoba, amesema ajali hiyo ilitokea Septemba 22, 2026, saa 9:15 mchana katika barabara kuu ya Lindi–Dar es Salaam.

Amesema ajali hiyo ilihusisha Toyota Coaster yenye namba za usajili T930 ERF, iliyokuwa ikiendeshwa na Halifan Cosmas Madodo (44), na lori aina ya Scania lenye namba za usajili T511 EPS, likiwa na tela namba T469 EPL, lililokuwa likiendeshwa na Hassan Salum Goro (30).

Kwa mujibu wa Mutayoba, watu wanane waliokuwa ndani ya Toyota Coaster walifariki dunia, huku wengine 12 wakijeruhiwa katika ajali hiyo.

Ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Coaster, ambaye alishindwa kulimudu gari lake na kusababisha kuhamia upande wa kulia wa barabara, ambako liligongana uso kwa uso na lori hilo.

Mutayoba amesema majeruhi wamepelekwa katika Kituo cha Afya Mohoro kwa ajili ya matibabu, huku baadhi yao wakitarajiwa kuhamishiwa katika hospitali kubwa kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Ametoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kusababisha vifo, majeraha na uharibifu wa mali.



Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...