Na Mwandishi wetu, Geita


VIJANA nchini wametakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali nchini ikiwemo madini, kilimo, ufugaji, teknolojia, uvuvi na ujasiriamali kwani vijana ni ajira.

Mkurugenzi mtendaji wa Youth Growth Foundation, Abdul Mzakiru ameeleza hayo kwenye maonyesho ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayofanyika manispaa ya Geita.

Mzakiru amesema kwenye maonyesho hayo ya Geita wanahamasisha vijana kupitia kauli mbiu yao ya 'Kamata fursa kijanja, madini ni mchongo.'

Amesema fursa zipo na zinawasubiri vijana wanaojituma na wanawakaribisha vijana wote kujiunga na Youth Growth Foundation ili waunganishwe na fursa mbalimbali.

"Wakijiunga na Youth Growth Foundation tutawawezesha wapate fursa za ajira, mafunzo, biashara, masoko na wadau watakaowasaidia kufikia malengo yao fursa ni kijana, kijana ni ajira," amesema Mzakiru.

Ameeleza kuwa taasisi hiyo hutoa fursa za elimu, mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali ili kuwajengea vijana maarifa na ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko na ajira na fursa za biashara.

"Lengo la taasisi yetu kunasaidia vijana, wanawake na makundi maalum, wanufaike na rasilimali zinazowazunguka na wainuke kiuchumi kwa manufaa yao binafsi yatakayochangia amani na utulivu," amesema Mzakiru.

Amesema Dira ya Madini 2030 'Madini ni Maisha na Utajiri' inalenga kuongeza utafiti wa kina wa jiosayansi hadi angalau asilimia 50, taarifa zitakazosaidia wachimbaji wadogo kuchimba kwa uhakika badala ya kubahatisha.

Amesema Dira ya Taifa 2050 inaipa madini nafasi ya kuongoza kutoa ajira kwa vijana, kupitia mradi wa MBT Mining for a Brighter Tomorrow ambapo kupitia vikundi vya vijana wanapata fursa leseni za uchimbaji.

"Ukijiunga leo unaanza safari ya kujiajiri na kuwa chanzo cha ajira kwa wengine, ambapo ofisi kuu zetu zipo Dodoma mjini mtaa wa uhindini, karibuni vijana wote," amesema Mzakiru.

Makamu Mwenyekiti wa Youth Growth Foundation Yazidu Bitika amesema taasisi hiyo inashirikiana na RM TZ Geological LTD katika kufanya utafiti wa kitaalamu na teknolojia kwenye uchimbaji madini.

Bitika amesema wanashirikiana na RM TZ Geological wanaotoa ushauri wa kitaalamu, taarifa sahihi za kijiolojia, upimaji na uchambuzi wa miamba na ukaguzi na uhakiki wa leseni.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...