Benki ya Exim Tanzania imeendelea kudhihirisha dhamira yake ya kushirikiana na jamii katika kuchochea maendeleo endelevu kupitia udhamini wake Mkuu wa Kitonga Marathon 2026, mbio zilizolenga kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kutangaza fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

Mbio hizo zilizofanyika chini ya kaulimbiu “Tunza Mazingira, Wekeza Kilolo” ziliwakutanisha washiriki na wadau mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha utunzaji wa mazingira, ushiriki wa jamii na kuangazia fursa za maendeleo zilizopo wilayani humo, ikiwemo katika sekta za kilimo, utalii na biashara za wenyeji.

Kama Mdhamini Mkuu, Benki ya Exim iliunga mkono mbio hizo kama sehemu ya dhamira yake pana ya kushirikiana na jamii na wadau katika masuala yanayochangia maendeleo endelevu.

Akizungumzia udhamini huo, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu, alisema udhamini huo unaakisi imani ya Benki kwamba jukumu lake haliishii katika kutoa huduma za kifedha pekee, bali linajumuisha pia kuunga mkono mipango inayowaunganisha wadau katika kutekeleza vipaumbele vya pamoja vya maendeleo.

“Mbio za Kitonga zinatoa fursa ya kuitangaza zaidi Kilolo na uwezo wake wa kiuchumi, huku zikihamasisha uwajibikaji wa pamoja katika uhifadhi wa mazingira. Sisi Exim Bank tunaamini kuwa maendeleo endelevu yanahitaji ushirikiano kati ya jamii, wafanyabiashara na wadau wengine. Udhamini wetu wa mbio hizi unaakisi dhamira yetu ya kushirikiana na jamii tunazozihudumia na kuchangia juhudi zinazolenga kuleta maendeleo katika maeneo yao,” alisema Kafu.

Udhamini huo ni sehemu ya jitihada za Benki ya Exim Tanzania za kuchangia maendeleo ya jamii kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii, Exim Cares. Kupitia mpango huo, Benki inaunga mkono shughuli mbalimbali zinazolenga kuboresha maisha ya jamii katika sekta za afya, elimu, uhifadhi wa mazingira, ubunifu na elimu ya masuala ya fedha.

Mwaka 2026, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 29 tangu kuanzishwa kwake, Benki ya Exim ilifanya shughuli za usafi katika jamii zinazozunguka matawi yake nchini. Mkoani Iringa, timu ya tawi la Benki hiyo ilikabidhi vifaa vya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya FLERIMO ili kusaidia kuboresha usafi katika hospitali hiyo.

Benki ya Exim Tanzania ilifungua tawi lake mkoani Iringa mwaka 2009. Tawi hilo hutoa huduma za kifedha kwa watu binafsi, wafanyabiashara, kampuni na taasisi, kulingana na mahitaji yao. Ushiriki wa tawi hilo katika Mbio za Kitonga unaonyesha namna Benki inavyoendelea kushirikiana na jamii inayohudumia pamoja na wadau wengine katika kuunga mkono mipango inayochangia maendeleo ya mkoa huo.

Kupitia Tawi lake la Iringa, Benki ya Exim Tanzania inaendelea kuwahudumia watu binafsi, wafanyabiashara na kampuni kwa kuwapatia huduma mbalimbali za kifedha. Wakazi na wamiliki wa biashara mkoani humo wanaweza kutembelea tawi hilo kupata maelezo kuhusu bidhaa na huduma za Benki, pamoja na ushauri kuhusu huduma zinazoweza kukidhi mahitaji yao ya kifedha.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...