Na Mwandishi Wetu, Mirerani
BENKI ya CRDB, Tawi la Mirerani wilayani Simanjiro, mkoani Manyara, imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kuwakutanisha wateja, mawakala na wafanyakazi wa benki hiyo kujadili masuala mbalimbali, yakiwemo fursa za kibiashara na namna ya kuboresha huduma.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Tanzanite Palace Hotel, Meneja wa CRDB Tawi la Mirerani, Renatus Rutajama, alisema kaulimbiu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka huu ni “The Extra Mile”, inayolenga kuwahamasisha watumishi kutoa huduma inayozidi matarajio ya wateja.
Rutajama aliwashukuru wateja waliojitokeza kushiriki katika hafla hiyo, akisema wameonyesha kuthamini uhusiano uliopo baina yao na benki.
“Leo ni siku ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja. Kuanzia Oktoba 5 kwa muda wa wiki nzima tunaadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja,” alisema.
Alisema dhana ya “The Extra Mile” inalenga kuhakikisha mteja anapofika benki kwa ajili ya huduma moja, anapatiwa pia taarifa na fursa za huduma nyingine zinazoweza kumsaidia kukidhi mahitaji yake.
“Kwa mfano, kama mteja amekuja benki kwa ajili ya kufungua akaunti, tunapaswa kwenda hatua ya ziada kwa kumweleza na kumpatia huduma nyingine zinazoweza kumfaa,” alisema.
Rutajama alisema katika maadhimisho hayo wamepokea maoni na mapendekezo kutoka kwa wateja kuhusu namna ya kuboresha huduma katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Simanjiro, yakiwemo Terrat na Naberera ambako hakuna matawi ya benki hiyo.
Alisema CRDB inaendelea kupanua huduma zake ndani na nje ya nchi, hivyo maoni ya wateja kuhusu maeneo yenye uhitaji wa huduma za benki yanazingatiwa.
“Tumepokea maelezo yao. CRDB ina matawi mengi hadi nje ya nchi, ikiwemo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Dubai na China. Hivyo, maeneo wanayoyataja hapa Simanjiro tutayafanyia kazi, ikiwemo uwezekano wa kufikisha huduma kupitia matawi au mawakala,” alisema.
Kwa upande wake, Afisa wa CRDB, Adam Mgaza, aliwataka wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kukutana mara kwa mara na wateja wao ili kusikiliza maoni yao na kuboresha huduma.
“Mpendwa mteja, Benki ya CRDB inakutakia heri ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. Ni fahari yetu kukuhudumia na kuendelea kukupatia huduma bora kila wakati,” alisema.
Naye Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Rozali, Mji Mdogo wa Mirerani, Padri Aristarki Tarimo, aliipongeza CRDB kwa kuwakutanisha wateja na watumishi wa benki hiyo katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Sheikh wa Wilaya ya Simanjiro, Ramia Ramadhani, alisema CRDB imekuwa ikitoa huduma nzuri kwa wateja na kuitaka benki hiyo kuongeza wigo wa huduma katika maeneo mengine ya wilaya hiyo, hususan Terrat na Naberera.
Kwa upande wake, mmoja wa mawakala wa CRDB Mji Mdogo wa Mirerani, Abraham Macha, alisema umoja, mshikamano na upendo baina ya benki na wateja ni muhimu katika kujenga mazingira mazuri ya utoaji huduma.
Alisema uhusiano mzuri baina ya benki na wateja unapaswa kuambatana na huduma bora na tabasamu ili kujenga imani na kuimarisha mahusiano ya kibiashara.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...