Na Mwandishi wetu, Geita
KAMPUNI ya uwekezaji ya Anglo Ashant Gold (GGML) imekuwa ikitumia mpango wa utoaji huduma kwa jamii (CSR) kupitia miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, elimu, kilimo na miundombinu kwa manufaa ya jamii.
Mkurugenzi wa uendekezaji na mahusiano wa mgodi huo, Gilbert Mworia ameeleza hayo kwenye kongamano la kujadili fursa za uwepo wa mgodi wa GGML uliofanyika ukumbi wa Mkapa kwenye maonyesho ya tisa ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayofanyika viwanja vya Dkt Samia Suluhu Hassan manispaa ya Geita.
Mworia amesema kampuni hiyo imekuwa na mchango katika maendeleo ya jamii kupitia ulipaji kodi na uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara, huduma za afya, elimu na uwekezaji katika kilimo ni miongoni mwa maeneo ambayo kampuni imekuwa ikichangia kama sehemu ya wajibu wake kwa jamii.
"GGML hutumia kati ya Sh13 bilioni na Sh15 bilioni kwa mwaka kufadhili taasisi, mashirika, Serikali na watu binafsi katika maeneo mbalimbali," amesema Mworia.
Amesema wanao wajibu kwa jamii inayowazunguka ili waendelee kupata ridhaa ya wananchi kufanya shughuli zao.
"Sisi kama kampuni huwa tunafanya uwajibikaji kwa jamii inayotuzunguka, si Geita tu bali maeneo mbalimbali hapa nchini,” amesema Mworia.
Amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita na Manispaa ya Geita, kampuni hiyo hutenga Sh9.2 bilioni kila mwaka kwa ajili ya miradi katika sekta za elimu, afya, miundombinu, barabara na maji.
Ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ushirikiano na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), ambapo kampuni hiyo imeingia mkataba wa miaka mitatu wa kusaidia watoto wenye matatizo ya moyo.
Amesema kampuni hiyo ina meli ya huduma za afya inayotoa huduma kwa wananchi wanaoishi katika visiwa 10 vya Ziwa Victoria, hususan katika mikoa ya Geita, Mwanza na Kagera.
"GGML imejenga zaidi ya madarasa 1,000, vituo vya afya na zahanati zaidi ya 150 pamoja na kuchangia ujenzi na uboreshaji wa hospitali," amesema Mworia.
Ameeleza kwamba mchango wa kampuni hiyo hauishii katika miradi ya kijamii pekee, bali unahusisha pia mchango wake katika uchumi kupitia uwekezaji, ajira, ununuzi wa bidhaa na huduma kutoka kwa kampuni za kizawa pamoja na ulipaji kodi.
Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Geita, wameipongeza kampuni ya GGML kwa namna inavyowezesha miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye jamii.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...