Na Mwandishi Wetu, Serengeti
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Massana Mwishawa, jana, Oktoba 5, 2026, amefanya ziara ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti kwa lengo la kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa katika hifadhi hiyo.
Katika ziara hiyo, Kamishna Mwishawa amekagua hatua za utekelezaji wa miradi hiyo ikiwa ni sehemu ya juhudi za TANAPA katika kuimarisha miundombinu ya uhifadhi na utalii pamoja na kuboresha mazingira ya huduma kwa wageni wanaotembelea hifadhi hiyo.
Miongoni mwa miradi aliyokagua ni Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa Serengeti (Serengeti National Park Golf Course), ambao umefikia hatua kubwa ya ukamilishaji na unatarajiwa kuzinduliwa katikati ya mwezi Oktoba mwaka huu.
Pia amekagua matengenezo ya Kituo cha Kuongozea Ndege katika Uwanja wa Ndege wa Seronera, pamoja na Kituo cha Kutolea Taarifa kwa Wageni cha Serengeti (Serengeti Visitor Center), kilichojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Ujerumani na kinatarajiwa kuzinduliwa Oktoba 7, 2026.
Mradi mwingine uliokaguliwa ni Daraja la Viboko, lililopo katika barabara ya Seronera–Naabi, ambalo ni miongoni mwa miundombinu muhimu inayosaidia usafiri ndani ya hifadhi hiyo.
Kwa mujibu wa TANAPA, matengenezo na uboreshaji wa miundombinu ya barabara na madaraja utasaidia kuimarisha shughuli za uhifadhi na utalii, pamoja na kupunguza athari zinazoweza kujitokeza wakati wa msimu wa mvua, hususan kutokana na hali ya hewa ya El NiƱo.
Ziara hiyo pia ilihusisha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Godwell Meng’ataki, ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Magharibi, pamoja na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Ismail Ismail, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...