MASHINDANO Ya Urembo Miss Dar zone yachukua sura mpya baada ya kuita Warembo 12 tu kutoka katika mashindano ya wilaya za Dar es Salaam .

Akizungumza na Michuzi  Muandaaji wa shindano la Miss Dar zone Ruth Urio Maarufu Kama Mama J'adore amesema kutokana na uzoefu wake wakuandaa mashindano mbalimbali huku akijinasibu kuwa warembo wengi wamepita katika mikono yake huku akitoa Miss Tanzania ambae amefanya vizuri hadi kufikia Miss World Sylvia buberwa ,hivyo kuhaidi kupitia mashindano hayo ya Miss Darzone wategemee Miss Tanzania atapatikana kutoka hapo.

"Mwaka huu tunatarajia kuwa na msimu mkubwa zaidi, wenye ushindani, burudani

na matukio mbalimbali yatakayotufikisha kwenye kilele cha safari hii ya Miss Darzone ambapo tutachukua Warembo 12 tu katika mashindano madogo ya mkoa wa Dar es Salaam ambapo kwa sasa tunasubiri mchakato wa kupatiwa kwao."

Muandaaji huyo ameongeza kuwa  warembo wataingia kambini mwezi Oktoba huku  kilele chake Novemba 12,2026 ambapo zawadi kwa atakaevikwa taji ataondoka na gari mpya ambayo itawekwa wazi hivi karibuni aina ya gari hiyo na thamani yake.

Pia amewaomba Wazazi na Walezi kuwaruhusu mabinti zao  kushiriki mashindano hayo ya Urembo kwani Urembo sio uhuni kama inavyotafsiriwa na baadhi ya watu badala yake Mashindano hayo yamekuwa yakitoa Wasichana ambao wamekuwa mfano wa kuigwa ,Viongozi wa Kitaifa na Wasaidizi wa Jamii zao.

Muandaaji wa shindano la Miss Dar zone Ruth Urio Maarufu Kama Mama J'adore akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam wakati akitangaza rasmi ufunguzi wa Shindano hilo huku akiwasisitiza Wazazi kuwaruhusu mabinti kushiriki katika shindano hilo
Picha ya Pamoja Muandaaji wa shindano la Miss Dar zone Ruth Urio akiwa na Wadhamini pamoja na Mawakala wa Mashindano ya Urembo kutoka Wilaya za Jijini Dar es Salaam

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...