Madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda katika Stendi Kuu ya Mabasi ya Mizengo Pinda mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili kulinda maisha yao na abiria wanaowahudumia.

Wito huo umetolewa Oktoba 13, 2026 na Sajenti wa Polisi Veronica Rumisha wakati akitoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva hao, ambapo amesisitiza umuhimu wa kuvaa kofia ngumu (helmet) kila wanapotumia pikipiki.

Amesema matumizi ya kofia ngumu husaidia kupunguza hatari ya kupata majeraha makubwa kichwani endapo ajali itatokea.

Aidha, Rumisha amewataka madereva hao kuacha tabia ya kuendesha pikipiki kwa mwendokasi na kubeba abiria zaidi ya idadi inayoruhusiwa kisheria, hali inayojulikana kwa jina la mshikaki.

Amesisitiza kuwa madereva wanapaswa kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani wakati wote wanapotekeleza shughuli zao za usafirishaji, akieleza kuwa kufanya hivyo ni muhimu katika kupunguza ajali na kulinda maisha ya watumiaji wote wa barabara.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...