Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma wameanza kushiriki semina maalumu ya itikadi ya Chama hicho, inayolenga kuwaongezea uelewa kuhusu misingi, maadili na masuala mbalimbali yanayohusu Chama.
Mafunzo hayo yameanza leo, Oktoba 9, 2026, na yanatarajiwa kuendelea hadi Oktoba 25, mwaka huu, yakihusisha makada kutoka wilaya mbalimbali za mkoa huo, ikiwa ni sehemu ya mafunzo yanayoendelea kutolewa kwa wanachama wa CCM nchini kote.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama wanaoshiriki mafunzo hayo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Kiliani Mwisho, amesema wamepokea mafunzo hayo kwa furaha, akieleza kuwa baadhi ya wanachama wamekuwa wakikosa fursa za kupata mafunzo ya aina hiyo kwa muda mrefu.
Mwisho, ambaye ameshiriki mafunzo hayo kama mwanafunzi katika darasa lililopo Kata ya Mjimwema, Wilaya ya Songea Mjini, ameipongeza CCM kwa kuandaa mafunzo hayo yanayolenga kuwajengea wanachama uelewa kuhusu itikadi na masuala ya Chama.
Pia, amempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha mafunzo hayo kufanyika nchi nzima, huku akimpongeza Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM, Kenani Laban Kihongosi, kwa uratibu wa mafunzo na maandalizi ya walimu wanaoyatoa kwa wanachama.
Kwa upande wake, Mratibu wa mafunzo hayo Mkoa wa Ruvuma, Edna Lameck, ambaye ni afisa wa Idara ya Itikadi na Uenezi kutoka Makao Makuu ya CCM, ametembelea madarasa mbalimbali yanayoendesha mafunzo hayo mkoani humo ili kujionea namna yanavyotolewa.
Lameck amesema ameridhishwa na hali ya utoaji wa mafunzo hayo kwa makada wanaoshiriki katika madarasa hayo mkoani Ruvuma.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 25, 2026, yakiwa na lengo la kuendelea kuwajengea uwezo viongozi, makada na wanachama katika kufahamu itikadi, siasa na misingi ya Chama Cha Mapinduzi.

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...