Kama ulikuwa bado unatafuta sababu ya kuweka pembeni mipango ya Oktoba 17, Marioo amekupa moja! Staa huyo wa Bongo Flava amejiunga na line-up ya 4Plays, sherehe za miaka minne ya 1245, zinazotarajiwa kufanyika Superdome Arena, Masaki.

Marioo, aliyeshinda tuzo ya Best Male East Africa kwenye AFRIMMA 2026, atapanda jukwaani akiwa na ushindi wa kimataifa wa kusherehekea pamoja na mashabiki wake. Tuzo tayari ipo, sasa ni zamu ya Dar kupiga kelele!

Ujio wake unaongeza msisimko kwenye line-up inayomjumuisha pia Young Jonn kutoka Nigeria. Kwa wanaopenda Bongo Flava na Afrobeats, hapo kisingizio cha “sio muziki wangu” kimeanza kukosa nguvu.

Kwa wanaojua vibes za 1245, fikiria ile energy ya club ikienda kwenye ukubwa wa Superdome, crew yako, muonekano wako wa weekend na nyimbo unazozijua mpaka mwisho. 4Plays inakuhakikishia Mega club experience, yenye live performances zinazokupa sababu ya kuacha simu mfukoni na kuzama kwenye muziki

Sherehe hizo zinaungwa mkono na Air Tanzania, Clouds Media, Johari Rotana, Heineken na Don Julio, huku 1245 ikiadhimisha miaka minne kupitia usiku wa muziki na burudani.

Tiketi zinapatikana kupitia 4plays.1245tz.com. Kwa ununuzi au maelezo zaidi, wasiliana kupitia 0748 211 245.

Marioo yupo, tarehe ipo, jukwaa lipo. Kilichobaki ni wewe kuamua utaimba mbele ya jukwaa au kupitia stories za wengine! Unaambiwa Hii ni chess sio checkers.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...