Na Victor Masangu, Pwani
WAZIRI wa Afya, Mohamed Mchengerwa, ametoa Sh milioni 35.1 kwa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani, ikiwa ni sehemu ya kuwaunga mkono katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa nyumba za makatibu wa jumuiya hiyo katika ngazi ya Mkoa na Wilaya.
Mchengerwa, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), ametoa mchango huo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kikao cha Baraza la Kawaida la UWT Mkoa wa Pwani, kilichowakutanisha viongozi mbalimbali wa chama na Serikali, wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo.
Akizungumza katika kikao hicho, Mchengerwa alisema ameamua kutoa mchango huo kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuimarisha jumuiya zao.
Alisema ataendelea kushirikiana na wanawake wa UWT kwa hali na mali, hususan katika kuwawezesha kutekeleza miradi ya maendeleo itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi na kupunguza utegemezi.
“Nimefarijika sana kualikwa katika kikao hiki cha Baraza la Kawaida la UWT Mkoa wa Pwani. Nimechangia Sh milioni 35.1 kwa ajili ya kuwasaidia wanawake katika mambo mbalimbali, ikiwemo miradi ya ujenzi wa nyumba za makatibu wa UWT katika ngazi za Wilaya na Mkoa,” alisema Mchengerwa.
Alisema anatamani kuona wanawake wakijenga uwezo wa kiuchumi na kuwa na miradi endelevu itakayowasaidia wao pamoja na jumuiya kwa ujumla.
Mchengerwa pia aliwahimiza wanawake wa Pwani kudumisha umoja, mshikamano na amani, akiwataka kuachana na tabia zinazoweza kuvuruga mshikamano wao na badala yake kuweka misingi imara ya kuimarisha jumuiya na chama.
MARIAM AKABIDHI PIKIPIKI 10
Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Mariam Ibrahimu, amekabidhi pikipiki 10 kwa UWT Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuanzisha miradi ya kuwaingizia kipato.
Mariam alisema ametumia sehemu ya fedha za mshahara wake kusaidia kuwawezesha wanawake kiuchumi, ambapo pikipiki hizo zitatumika kama kitega uchumi katika jumuiya hiyo.
Alisema pikipiki hizo zitatumika katika ngazi mbalimbali za UWT, huku akisisitiza kuwa lengo ni kuwawezesha wanawake kuanzisha miradi itakayowasaidia kujitegemea na kuondokana na utegemezi.
“Nimeamua kutumia fedha zangu za mshahara kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wa Mkoa wa Pwani. Nimekabidhi pikipiki 10 ambazo zitasaidia jumuiya za wanawake katika Wilaya mbalimbali na kuwawezesha kujikwamua kiuchumi,” alisema Mariam.
Mbali na pikipiki hizo, Mariam pia alikabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh milioni 20 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa miradi ya ujenzi ya UWT Mkoa wa Pwani.
UWT YAPANIA KUJITEGEMEA
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani, Zainabu Vullu, alisema jumuiya hiyo imeweka mikakati ya kuondokana na utegemezi kwa kuanzisha na kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo yenye tija kwa wanawake.
Alisema lengo ni kuhakikisha UWT inakuwa na miradi endelevu itakayowezesha jumuiya hiyo kujiendesha na wakati huo huo kuwasaidia wanawake kiuchumi.
Naye Katibu wa UWT Mkoa wa Pwani, Aziza Omary, alisema wamejiandaa kutekeleza mipango mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa nyumba za makatibu wa UWT katika ngazi ya Mkoa na Wilaya.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, aliwataka wanawake kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali, ikiwemo mikopo ya asilimia 10 inayotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi.
Alisema wanawake wanapaswa kutumia fursa hizo kuanzisha na kuendeleza miradi yenye tija badala ya kuendelea kuwa tegemezi.
Katika kikao hicho, wajumbe walijadili masuala mbalimbali, ikiwemo uanzishwaji na uendelezaji wa miradi ya maendeleo, ujenzi wa nyumba za makatibu wa UWT katika ngazi ya Mkoa na Wilaya, mikakati ya kuimarisha jumuiya na uhai wa wanachama, pamoja na namna bora ya kutumia pikipiki walizopewa kama vitega uchumi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...