Na Mwandishi Wetu, Arusha

WAZIRI wa Afya, Mohammed Mchengerwa, amewataka wafamasia na wataalamu wa dawa nchini kuzingatia maadili ya taaluma na kuhakikisha viwanda vya dawa vinavyojengwa nchini vinazalisha dawa salama na zenye ubora unaokidhi viwango vinavyotakiwa.

Mchengerwa ameyasema hayo leo, Oktoba 27, 2026, jijini Arusha, wakati akifungua Kongamano la 27 la Chama cha Wateknolojia Dawa Tanzania (TAPHATA), akisisitiza kuwa kuimarisha uzalishaji wa dawa nchini kutapunguza utegemezi wa bidhaa hizo kutoka nje, kuongeza ajira na kukuza uchumi wa taifa.

Amesema Serikali inalenga kuhakikisha Tanzania inazalisha asilimia 70 ya mahitaji yake ya dawa ifikapo mwaka 2030, hatua inayohitaji ushirikiano kati ya Serikali, wawekezaji, taasisi za udhibiti na wataalamu wa dawa.

Amesisitiza kuwa wataalamu hao hawapaswi kushawishiwa na maslahi binafsi yanayoweza kuhatarisha ubora na usalama wa dawa, akibainisha kuwa jukumu lao kuu ni kulinda afya za Watanzania.

Ameongeza kuwa kukua kwa viwanda vya dawa kutafungua fursa za ajira katika maeneo mbalimbali, yakiwemo uzalishaji, utafiti, uhakiki wa ubora, usajili wa bidhaa na usimamizi wa ugavi wa dawa.

Kwa upande wake, Rais wa TAPHATA, Thabiti Milandu, amesema kongamano hilo ni fursa kwa wataalamu kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto za sekta na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuboresha taaluma, usalama wa dawa na upatikanaji wa huduma bora za afya.

Milandu amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya wataalamu, taasisi za Serikali, vyuo vya mafunzo, sekta binafsi na wadau wa maendeleo ili kukuza viwanda vya ndani na kuhakikisha vinakidhi mahitaji ya soko.

Aidha, ameeleza kuwa kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza fursa za mafunzo endelevu kutawajengea uwezo wataalamu wa dawa kushiriki kikamilifu katika uzalishaji na matumizi ya teknolojia za kisasa, huku kukipanua wigo wa ajira katika sekta ya umma na binafsi.

Naye Mfamasia wa Viwanda kutoka Wizara ya Afya, Felista Rugarabamu, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ujuzi wa wataalamu wa Kitanzania katika uzalishaji wa dawa, utafiti na matumizi ya teknolojia za kisasa.

Amesema uwekezaji katika mafunzo, utafiti na uhamishaji wa teknolojia utasaidia kuongeza uwezo wa viwanda vya ndani, kupunguza changamoto ya upatikanaji wa wataalamu wenye ujuzi maalumu na kuimarisha uzalishaji wa dawa zinazokidhi viwango vya ubora na usalama.

Ameongeza kuwa ushirikiano endelevu kati ya Serikali, wataalamu wa dawa na sekta binafsi ni muhimu katika kujenga tasnia imara itakayokidhi mahitaji ya ndani na kupanua fursa za soko la kikanda.

Waziri wa Afya,Mohammed Mchengerwa akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wadhamini wa Kongamano la 27 la Chama cha Wateknolojia Dawa Tanzania (TAPHATA) jijini Arusha.

Wajumbe wa Kongamano la 27 la Chama cha Wateknolojia Dawa Tanzania (TAPHATA) jijini Arusha.
Waziri wa Afya,Mohammed Mchengerwa akifungua Kongamano la 27 la Chama cha Wateknolojia Dawa Tanzania (TAPHATA) jijini Arusha.


Mfamasia wa Viwanda kutoka Wizara ya Afya, Felista Rugarabamu akiwasilisha mada wakati wa kongamano hilo jijini Arusha.

Wajumbe wa Kongamano la 27 la Chama cha Wateknolojia Dawa Tanzania (TAPHATA) jijini Arusha.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...