Na Mwandishi wetu, Geita

KAMPUNI ya MINETEC inayohusisha na uuzaji wa vifaa vya uchimbaji madini imekuwa fursa kubwa kwa wachimbaji madini hususan ya dhahabu kwa kanda ya ziwa kupata vipuri kwa urahisi.

Meneja masoko wa kampuni ya MINETEC, Khalid Adinan Ajali ameeleza hayo akizungumza mbele ya mgeni rasmi wa maonyesho hayo Peter Louis Bura aliyetembelea banda lao.

Khalidi amesema kwenye maonyesho hayo wamekuja na baadhi ya vifaa walivyonavyo vya uchimbaji madini na vinapatikana hapo.

"Hapa kuna Compressor ya diesel na umeme, Water pump, Jak hammer bum bum digger, Escaveter JCB Hydrolics na spare parts," amesema Khalidi.

Meneja masoko msaidizi wa kampuni ya MINETEC, Irene Munna amesema wanasambaza vifaa vya uchimbaji madini kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo mikoa ya kanda ya ziwa.

" Tunawafikia wachimbaji wa madini ya dhahabu ikiwemo Geita, Mwanza, Musoma Mara kule Buhemba na hata makao makuu ya nchi Dodoma tunawafikia," amesema Munna.

Mgeni rasmi wa maonesho hayo kwa siku hiyo, Peter Louis Bura akizungumza kwenye banda hilo amewapongeza MINITEC kwa kuwa na vifaa hivyo vinavyosaidia wachimbaji.

Bura amesema ametembelea banda la kampuni ya MINETEC na kuvutiwa na vipuli mbalimbali vilivyopo eneo hilo katika maonyesho hayo ya tisa ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayofanyika viwanja vya Dkt Samia Suluhu Hassan manispaa ya Geita.

"Mimi binafsi nimevutiwa na pampu ya kuvutia maji ya thamani ya shilingi milioni 1.6 Pump Model: QX12.5-60-5.5 7.5HP ya mita:60 yenye ubora kabisa," amesema Bura.

Amesema wachimbaji madini watafaidika kupitia fursa hizo za kampuni ya MINETEC na kauli mbiu ya mwaka 2026 ya maonyesho ya tisa ya kitaifa ya teknolojia ya madini ni 'Madini ni Utajiri, tuwajibike kwa pamoja kufikia Dira ya Taifa 2050' amesema Bura.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...