Na Farida Mangube, Morogoro
Mkwawa Group of Campaign imekabidhi kisima chenye thamani ya Sh milioni 38 kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), katika eneo la Makunganya, mkoani Morogoro.
Kisima hicho kinatarajiwa kutumika katika shughuli za uhifadhi, ikiwemo kuotesha na kulea miche ya miti, sambamba na kuwasaidia wananchi wa maeneo ya jirani ambao awali walilazimika kutembea umbali wa hadi kilomita 10 kutafuta maji safi na salama.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi kisima hicho, Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Kiwanda cha Mkwawa, David Mayunga, amesema kampuni hiyo imeamua kuunga mkono shughuli za uhifadhi zinazotekelezwa na TFS.
Mayunga amewataka wananchi kukitunza kisima hicho ili kiendelee kutoa huduma kwa muda mrefu na kunufaisha jamii pamoja na shughuli za uhifadhi.
Kwa upande wake, Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Morogoro na Mkuu wa Kituo cha Uzalishaji Mbegu za Miti, Mohamed Msalu, amesema kisima hicho kimewasili kwa wakati muafaka kutokana na mkakati wa TFS wa kuongeza uzalishaji wa mbegu na miche ya miti.
Amesema uwepo wa kisima hicho pia utapunguza changamoto ya upatikanaji wa maji kwa jamii inayozunguka shamba hilo na kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi na wahifadhi.
Msalu ameishukuru Mkwawa Group of Campaign kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika uhifadhi na utalii ikolojia, akisema miundombinu hiyo itasaidia pia shughuli mbalimbali za uhifadhi ndani ya shamba.
Naye, Recho Mapenza, mkazi wa Makunganya, ameishukuru TFS na Mkwawa Group of Campaign kwa kuwezesha upatikanaji wa kisima hicho, akisema kimewapa unafuu wananchi waliokuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji.
Amesema wananchi wataendelea kushirikiana na TFS katika kukitunza kisima hicho pamoja na kulinda mazingira yanayowazunguka.

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...