HANDENI, Tanga
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Oktoba 4, 2026, anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Ibada ya Misa Takatifu ya kuwekwa wakfu kwa Kasisi na Canon Charles Mika Lundu kuwa Askofu wa Dayosisi ya Handeni.
Ibada hiyo pia imeambatana na uzinduzi rasmi wa Dayosisi ya Handeni, iliyotenganishwa na Dayosisi ya Tanga.
Ibada hiyo inafanyika katika Kanisa Kuu la Anglikana Kristu Mfalme, Chanika, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Uwekaji wakfu wa Askofu Lundu unaashiria hatua muhimu katika kuanza rasmi kwa shughuli za Dayosisi ya Handeni, huku viongozi wa Serikali, viongozi wa dini na waumini wakishiriki katika tukio hilo.



.jpeg)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...