Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Sanaa na Michezo, Mwana Fa, amepokea na kutunukiwa nakala ya riwaya ya Garasa, iliyoandikwa na mwandishi Laura Pettie Kissakwa, katika tukio lililoambatana na ubadilishanaji wa saini za kipekee kati ya mwandishi huyo na Naibu Waziri.

Katika hafla hiyo, Laura Pettie alikabidhi nakala ya Garasa kwa Naibu Waziri na kusaini kitabu hicho kwa autograph yake kama mwandishi wa kazi hiyo.

Kwa upande wake, Mwana Fa aliweka autograph yake katika nakala hiyo kwa kutumia kalamu yenye wino wa kijani, ikiwa ni ishara ya heshima na kumbukumbu ya kupokea kazi hiyo ya kifasihi.

Tukio hilo limeifanya nakala hiyo kuwa na kumbukumbu ya kipekee kutokana na kusainiwa na wahusika hao wawili katika nafasi zao tofauti, Laura Pettie kama mwandishi wa riwaya na Mwana Fa kama Naibu Waziri wa Sanaa na Michezo pamoja na msanii wa muziki.

Kwa mujibu wa mwandishi, makabidhiano hayo yanaipa Garasa nafasi nyingine katika safari yake ya kutambulika na kuthaminiwa katika medani ya fasihi na sanaa nchini, huku yakifungua fursa ya kazi hiyo kuhusishwa zaidi na wadau wa sanaa na utamaduni.

Garasa ni riwaya iliyotokana na muswada ulioshinda Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere katika kipengele cha Riwaya mwaka 2024. Kitabu hicho kilizinduliwa rasmi mwaka 2026 na Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda, na kimesambazwa na kinaendelea kusomwa katika shule za sekondari za Serikali nchini.

Makabidhiano hayo pia yanaonesha namna fasihi na muziki zinavyoweza kukutana kupitia sanaa, huku saini za pande zote zikibeba kumbukumbu ya mwingiliano kati ya mwandishi wa riwaya na msanii anayeshika nafasi ya uongozi katika sekta ya sanaa.

Tukio hilo ni sehemu ya jitihada za kuendelea kutambua na kuenzi kazi za waandishi wa Tanzania pamoja na kuimarisha uhusiano kati ya fasihi na sanaa kwa ujumla.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...